MHE. WASIRA AIPONGEZA MENEJIMENTI YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mhe. Stephen Wasira ameipongeza Menejimenti ya Chuo hicho kwa Kujenga ofisi za Walimu na kumbi za Mihadhara kwa kutumia Makusanyo ya Mapato ya ndani, na hivyo kusaidia kupunguza changamoto ya Ofisi na Madarasa iliyokuwa inaikabili Taasisi hiyo. Mhe. Wasira ameyasema hayo leo baada ya kuzindua jengo lenye ofisi zinazoweza kutumiwa na Walimu zaidi ya Sabini na kumbi mbili za Mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi Mia sita kwa mara moja kwa kila kumbi. Kwa upande wake Mkuu wa ... huo Prof. Haruni Mapesa amesema kuzinduliwa kwa ofisi na kumbi za Mihadhara kutasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa vyumba vya kufundishia na ofisi ambazo zitatumiwa na Watumishi. Mkuu huyo wa Taasisi amebanisha kuwa dhamira kuu ya ujenzi huo ni kuboresha ustawi na kutoa huduma bora kwa Wanafunzi na Wafanyakazi. Ameongeza kuwa ujenzi huo utasaidia kuongeza mapato ndani ya Taasisi kwani chuo kitaongeza udahili wa Wanafunzi pamoja na kuendeleza mazingira bora, rafiki na safi kwa Ustawi wa jamii ya Chuo. Mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni Moja na Milioni Sitini na Saba. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 21.05.2026 Read more >
[ 2026-05-22 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam
W
E
L
C
O
M
E