WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA MNMA
Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda leo ametembelea Banda la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika maonesho ya VETA yanayoendelea katika viwanja vilivyopo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam( JNICC). Mhe. Mizengo Pinda amekipongeza Chuo kwa kushiriki maonesho hayo, ambapo amejionea bunifu mbalimbali za Wanafunzi wa Chuo na kusema kuwa anatambua mchango unaotolewa na Chuo hicho. “Nakifahamu vizuri Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,ambapo muasisi wake ni baba wa Taifa na kilianzish ... a kwa lengo la kuwaandaa viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali”, alisema Mhe. Mizengo Pinda. Mhe. Pinda alipongeza kazi mbalimbali alizojionea kutoka kwa wabunifu wa Chuo hicho na kuvutiwa na ubunifu wa mfumo wa namna kuandaa Kitalu cha mbegu za mpunga ( trans- plant cultivation alert system) Maonesho hayo ya VETA yanafanyika ikiwa ni sehemu ya Taasisi hiyo kutimiza miaka 30,ambapo kesho tarehe 21 Maadhimisho yatafikia kilele. Imeandaliwa na : Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 20.03.2025 Read more >
[ 2025-03-20 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam