SERIKALI YA WANAFUNZI WATAKIWA KUZINGATIA MISINGI YA UONGOZI NA UTAWALA BORA
Viongozi wapya wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), walioteuliwa kwa mwaka wa masomo 2025/26 wametakiwa kuzingatia misingi ya Uongozi na Utawala bora, Uwazi na Uongozi unaofuata Sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Akizungumza leo katika hafla fupi iliyofanyika Chuoni hapo Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Haruni amesema uongozi bora ni ule unaoshirikisha watu katika ufanyaji wa maamuzi kwa pamoja na kwa kufuata misingi ya kuongoza. Prof. Mapesa amesema Kazi ya U ... ngozi si ndogo hivyo amewapongeza wote waliochaguliwa kuongoza serikali ya wanafunzi na wale wote walioshiriki uchaguzi mkashirikiane kwa pamoja na kuwa mabalozi wapya na kuhakikisha wanakisemea vizuri Chuo. Mkuu huyo wa Chuo pia amempongeza Rais aliyemaliza muda Barick Mtawa kwa uongozi wake, huku akimuahidi Rais mpya wa Wanafunzi aliyechaguliwa kuwa atapata ushirikiano wa kutosha katika utendaji wa kazi zao kutoka katika Menejimenti ya Chuo. Rais mpya wa Serikali ya Wanafunzi Magashi Magina ameshukuru Uongozi wa Chuo kwa ushirikiano ambao wameuonesha kuanzia mchakato wa Uchaguzi hadi matokeo, hivyo ameahidi kutoa ushirikiano kwa Menejimenti ya Chuo, Wafanyakazi na Wanafunzi wakati wote atakapokuwa anatumikia nafasi hiyo. kwa upande wake Rais aliyemaliza muda wake Barick Mtawa alisema viongozi wapya wakawe daraja kati ya Serikali ya wanafunzi na Menejimenti na kufuata misingi na miongozo ya chuo kwa kujiepusha na migomo ya aina yeyote, pia ameishukuru Menejimenti kwa ushirikiano alioupata yeye pamoja na serikali katika kipindi chote cha uongozi wao. Viongozi waliochaguliwa ni Magashi Magina nafasi ya Rais wa Serikali ya wanafunzi MASO, na Makamu wa Rais ni Tausi Dipunga ambao wataongoza Serikali ya wanafunzi kwa mwaka 2025/26. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 26.05.2025. Read more >
[ 2025-05-27 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam