MAPESA AITAKA SERIKALI YA WANAFUNZI KUTUMIA FURSA ZA MAFUNZO KUJIFUNZA KUWA VIONGOZI BORA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Prof. Haruni Mapesa ameitaka Serikali mpya ya Wanafunzi wa Chuo (MASO), kuzingatia, kujifunza kwa weledi na kuyatumia mafunzo watakayoyapata katika semina elekezi ya kuwajengea uwezo ili wawe viongozi bora na wa kuigwa katika kipindi chote cha uongozi wao. Hayo ameyasema Mkuu wa Chuo Prof. Mapesa Wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo serikali mpya ya wanafunzi kwa mwaka 2025/26 yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kampasi ya Kivukoni. ... Prof. Mapesa amesema mafunzo watakayoyapata wakayatumie katika kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kuishi viapo vyao walivyoapa baada ya kuteuliwa kuongoza serikali ya wanafunzi wa chuo hicho. “ Serikali ya wanafunzi (MASO) ni daraja kati ya wanafunzi na Menejimenti ya Chuo katika kuwasilisha maoni, kero, changamoto zinazowakabili wanafunzi hapa chuoni, hivyo mafunzo haya yatawajenga katika kutambua misingi ya sheria na taratibu za kufuata katika kuwasilisha mambo mbalimbali katika menejimenti”, Alisisitiza Prof. Mapesa. Mkuu huyo wa Chuo pia ameitaka Serikali ya wanafunzi kuwa mfano wa kuigwa kwa wenzao katika kuwashawishi kusoma kwa bidii ili kujiepusha na vitendo vya udanganyifu katika kipindi cha mitihani, kuwashawishi wanafunzi wenzao katika ulipaji wa ada pamoja na michango mbalimbali ya chuo, na kujiepusha na makundi ya migogoro katika muda wao ili waweze kuyafikia malengo ya kumaliza chuo kwa pamoja. Baadhi ya mada zitakazowasilishwa ni pamoja na Dhana ya Uongozi na Utawala Bor. Kanuni, Taratibu na Matumizi ya Fedha za Umma. Migogoro, Utatuzi, na Wajibu wa Serikali ya Wanafunzi. Mada nyingine zitakazowasilishwa ni Uongozi Bora, Maadili, Haki na Wajibu wa Kiongozi Bora, Mawasiliano na Matumizi ya Muda, na Kazi za Dawati la Jinsia. Semeni hiyo elekezi kwa Serikali mpya ya Wanafunzi ni maalumu katika kuwajengea uwezo viongozi wa serikali hiyo ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na weledi katika muda wote wa uongozi wao. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 12.06.2025 Read more >
[ 2025-06-13 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam