PROF. MAPESA AMEWATAKA WANATAALUMA WA MNMA -KUFANYA TAFITI ILI KUONGEZA MAPATO YA CHUO
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa amewataka Wanataaluma wanaoshiriki semina ya kujengewa uwezo wa namna ya kupata miradi mikubwa ya tafiti kuhakikisha wanatumia nguvu ya kutosha katika kuandika na kufanya machapisho, pamoja na kutoa Ushauri wa kitaalamu ili kukiongezea Chuo mapato, na kukupandisha Chuo kuwa katika hadhi ya juu. Prof. Mapesa ameyasema hayo leo wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wanataaluma "Namna ya kupata miradi mikubwa ya tafiti na ushauri wa kitaalamu" na kuwa semina hiyo maalumu i ... awahusu wanataaluma waliochaguliwa kutoka idara mbalimbali kwa kampasi ya Kivukoni, Karume na Pemba. Prof. Mapesa amesema anaamini wanataaluma wakiondoa ubinafsi,na utengano wataweza kukiwakilisha Chuo vizuri hivyo mafunzo hayo ni muhimu kwao na kwa Taasisi pia. “ Niwasihi sana kuendelea kufanya machapisho kwa Maslahi ya Taasisi na kwa Maslahi ya mtu mmojammoja na hapa nisisitize kuhakikisha tunafanya machapisho, na pia machapisho hayo yakitoka basi ni vyema mtu huyo akapandishwa daraja”, Alisisitiza Prof. Mapesa. Mkuu huyo wa Chuo Alisisitiza kuwa fedha inayopatikana kwa Utafiti na Ushauri wa kitaalamu pia inasaidia kuimarisha hali ya Miundombinu na kutatua changamoto mbalimbali katika Taasisi. Pia Prof. Mapesa amewataka Wanataaluma hao kuhakikisha wanashirikisha vyombo vya Habari ili visaidie kutangaza kazi kubwa zinazofanywa na Chuo kuhusu masuala ya Tafiti na Ushauri wa Kitaalamu, pia inakuwa ni sehemu ya kukitangaza Chuo. Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo, anaesimamia Taaluma na Ushauri wa Kitaalam Prof. Richard Kangalawe amesema utafiti na Ushauri wa Kitaalamu ni moja ya kazi na majukumu ya Chuo, hivyo jukumu la watafiti ni kutengeneza Maarifa ndiyo maana semina hiyo inafanyika ili kujengeana uwezo kwa ajili ya siku zinazokuja. Naye Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala Dkt. Evaristo Haulle amesema kuwa kuwajengea uwezo wanataaluma hao ni sehemu ya kutekeleza bajeti ambayo ni sehemu ya majukumu ya ofisi anayoisimamia, hivyo amewataka Washiriki kujifunza na kuzingatia ili mrejesho wa mafunzo hayo uwe ni Taasisi kupata Miradi mikubwa kwa Maslahi mapana ya Chuo. “Huu ni uwekezaji na marejesho yake ni Taasisi kupata mapato ambayo yatapatikana kutokana na Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu”,alisema Dkt . Haulle. Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Washiriki wa mafunzo hayo ya kujengewa uwezo kwenye masuala ya tafiti na Ushauri wa Kitaalamu Dkt. Rose Mbwete Mkurugenzi wa Kampasi ya Karume amemshukuru Mkuu wa Chuo kwa kukubali na kuidhinisha mafunzo hayo yafanyike, ambapo ameahidi kwa niaba ya Wanataaluma wengine kuwa watazingatia mafunzo hayo na matokeo chanya yatapatikana. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 16.06.2025 Read more >
[ 2025-06-18 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam