|
|
|
PROF. KANGALAWE AFUNGUA MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI KWA WANAFUNZI WAHITIMU -MNMA
Kaimu Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma, Prof. Richard Kangalawe, jana Julai 27,2026 amefungua Mafunzo ya muda Mfupi ya Uongozi na Maadili kwa Wanafunzi waohitimu Programu mbalimbali za mafunzo katika ngazi ya Cheti, Diploma na Shahada katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Akifungua Mafunzo hayo ya siku tatu Prof. Kangalawe amewataka Wanafunzi hao wanaohitimu kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili na weledi kuwajibika katika kuihudumia jamii na taifa kwa ujumla, kuwa w ...
zalendo na kuhakikisha wanakuwa ni mfano wa kuigwa na wengine katika jamii wanazoishi.
Kaimu Mkuu huyo wa Chuo amesema, lengo la Kuanzishwa kwa Chuo wakati huo ilikuwa ni kuwaandaa Viongozi ili waweze kushika nyadhifa mbalimbali za Uongozi katika nchi, lengo ambalo bado linaendelezwa hata sasa. Hivyo, Mwanafunzi anayemaliza katika Chuo hiki ni lazima awe wa tofauti kwa sababu ana maarifa ya ziada anayoyapata katika mafunzo ya Uongozi na Maadili. Amewaasa kuwa mabalozi wazuri wa Chuo kwa kuzingatia misingi ya utu, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji na mfano mwema popote watakapokuwa baada ya kuhitimu.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Evaristo Haulle, amewasisitiza Wanafunzi Wahitimu kuhakikisha wanajenga taswira nzuri ya Chuo kwa kuwa vijana bora na wenye Maadili mema, na kuhakikisha wanakitangaza vizuri Chuo kwa kuwa wao tayari wana mafunzo ya msingi kabisa yanayohusu Uongozi na Maadili.
Mtiva wa kitivo cha Uongozi na Maadili Dkt. Adili Zella ameelezea umuhimu wa Mafunzo hayo kwa Wanafunzi wanaohitimu kuwa ni kuwajengea uwezo katika kuimarisha uelewa katika nyanja zote za Maisha, Kuwahamisha kuwa Viongozi wenye Mawazo na mwelekeo chanya na kuweka maslahi ya Taifa mbele.
Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi Nasir Samir amewataka Wahitimu hao kuhaikisha wanakuwa nguzo kuu katika kuilinda na kujenga amani ya taifa na wasikubali kutumika vibaya kwani tayari mafunzo waliyoyapata kutoka Chuoni ni nguzo muhimu katika maisha yao yote.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Read more >
[ 2026-07-30 ]
|
|
|
|