PROF. MAPESA AONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI
Mkutano wa Kumi na Nne wa Baraza la Wafanyakazi umefanyika leo ukiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa. Kupitia Mkutano huo Wajumbe wa baraza walijadili taarifa ya utekelezaji wa Malengo na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Kupitia Mkutano huo wa baraza la wafanyakazi Wajumbe walichagua Mjumbe Mwakilishi wa baraza la Wafanyakazi katika Bodi ya Chuo ambapo Majina Matatu Kati ya matano yaliyochaguliwa ni Geofrey Malila, Moshi Machage na Felister Masasi ambapo majina hayo yatawasil ... ishwa Wizarani kwa hatua zaidi. Uchaguzi huo unatokana na aliyekuwa Mjumbe Mwakilishi Ally Kibona kumaliza muda wake wa uwakilishi katika bodi hiyo. Pia Mkutano huo wa Kumi na Nne umemchagua Esther Sanga kuwa katibu Msaidizi wa baraza la Wafanyakazi, Baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Jovita Rwezaula kuhamia Taasisi nyingine. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 28.08.2026 Read more →