Latest News

PROF. MAPESA AZINDUA KITIVO KIPYA CHA UCHUMI NA TAALUMA ZA BIASHARA

Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa amezindua kitivo kipya cha Uchumi na Taaluma za Biashara hatua inayolenga kuendana na ushindani katika soko la ajira pamoja na kukidhi mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Prof. Mapesa amesema hayo katika hafla fupi ya uzinduzi wa kitivo kipya cha Uchumi na Taaluma za biashara iliyofanyika katika Kampasi ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika uzinduzi huo wa Kitivo hicho Prof. Mapesa amesema kuwa kuanzishwa kwa kitivo hicho ni matokeo ya Chuo kukua, idadi ya Wana ... funzi kuongezeka na idadi ya watumishi wanaotoa huduma kuongezeka pia. Prof. Mapesa amewasisitiza watendaji wa kitivo hicho kuhakikisha wanafanya kazi kwa Umoja, kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora,na na kuhakikisha kozi za kitivo hicho zinatangazwa ili kufikia malengo ya Taasisi. Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amesema kitivo kinapaswa kuzingatia ubora wa hali ya juu katika eneo la Uchumi na taaluma za biashara, pamoja na kusimamia kwa weledi maeneo matatu ambayo ni taaluma, Utafiti na Ushauri wa kitaalamu. Naye Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Haulle alisisitiza kuwa kitivo hicho kinapaswa kufundisha na kusimamia nidhamu ya fedha kwa vitendo huku kikizingatia uwazi na uwajibikaji. Kaimu Mtiva wa kitivo hicho Dkt. Philip Daninga amesema uzinduzi wa kitivo hicho ni hatua katika kihistoria ya Chuo, ambapo ameahidi kufanya kazi kwa uwazi, uwajibikaji na ushirikiano wa dhati na watumishi wenzake ili kupanua wigo wa fursa mbalimbali kwa watumishi na wanafunzi wa kitivo hicho. Imetolewa na; Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 2.09.2026 Read more →