MNMA YATOA MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI KWA KANISA LA UFUNUO.
Wahadhiri wa Idara ya Uongozi na Maadili ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wameendesha Mafunzo ya Uongozi na Maadili ya siku moja kwa viongozi wa Kanisa la Ufunuo Tanzania lililopo Yombo Buza Kipera, jijini Dar es salaam. Lengo la Mafunzo hayo ni kuwaongezea uelewa katika misingi ya Uongozi, Maadili, Uzalendo na Uwajibikaji unafuata misingi,Kanuni na taratibu za nchi. Akizungumza katika mafunzo hayo Mkuu wa idara ya Uongozi na Maadili Dkt. Ambiliasia Mosha amesisitiza kuwa uzalendo unapaswa kwenda sambamba na kuzingatia haki na wa ... jibu wa kila mmoja kwa Taifa. Kwa upande wao Wahadhiri Waandamizi wa idara hiyo Dkt. Willy Maliganya na Dkt. Samwel Lunyelele wamezungumzia umuhimu wa itifaki na diplomasia, wakisisitiza juu ya uelewa wa taratibu, namna ya kuwasiliana na kushughulika na watu katika mazingira mbalimbali, pamoja na kujenga mahusiano yenye heshima na weledi. Naye Askofu Yaspi Bendera amekipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuona umuhimu wa kuwafikishia viongozi mafunzo hayo kupitia wataalamu wake, ambapo ametoa wito kwa Taasisi nyingine kutumia fursa hiyo ya kupata mafunzo hayo muhimu, Mafunzo hayo pia yameshirikisha Maafisa kutoka Jeshi la Polisi Tanzania. Mafunzo hayo ya siku moja yameratibiwa na Timu ya Wahadhiri kutoka idarao ya Uongozi na Maadili ya MNMA. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 10.09.2026 Read more →