Latest News

PROF. MAPESA AFUNGUA KONGAMANO LA TANO NA KUZINDUA KITABU CHENYE MKUSANYIKO WA MAKALA ZA KITAALUMA

Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. haruni Mapesa leo amezindua kitabu kinachohusu kumuenzi hayati baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere katika kongamano la Tano la Kitaaluma lililofanyika katika Kampasi ya Kivukoni jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati akizindua kitabu hicho Prof. Haruni Mapesa amewaalika watanzania na wanazuoni kutumia hazina kubwa ya Machapisho ya Vitabu vilivyopo katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili kupata maarifa ya kifalsafa, Maono na Itikadi mbalimbali ambazo baba wa Taifa aliishi nazo. ... Prof. Mapesa amesema kuwepo kwa kongamano la kumtafakari baba wa Taifa inatoa fursa kwa wadau mbalimbali kuyajadili na kuyapitia yale yote yaliyofanywa na Muasisi wa Taifa la Tanzania, kwa lengo la kuyaenzi na kuyaendeleza. Mkuu huyo wa Chuo aliitaja Mada kuu ya Kongamano hilo kuwa ni “URITHI WA MWALIMU NYERERE KATIKA UJENZI WA JAMII HIMILIVU NA ZINAZOJITEGEMEA KATIKA DUNIA INAYOBADILIKA.” Kwa upande wake Profesa Joel Norbert mmoja wa watoa mada katika Kongamano hilo alisema mabadiliko ya tabia nchi yanachangiwa na ongezeko la idadi ya watu inachangia kuwepo kwa uharibifu wa mazingira, hivyo wanadamu wanatakiwa kujua nmana bora ya kukabiliana na madiliko hayo. Naye Prof. Kalafunja Osaki amewataka Watanzania kuendelea kudumisha mila na desturi ili kuenzi misingi ya kihistoria iliyokuwepo toka enzi za baba wa taifa na kuacha kuiga mila za kisasa zisizokuwa na tija kwa Taifa. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 16.10.2026 Read more →