MNMA YAZINDUA BASI JIPYA KUBORESHA HUDUMA ZA USAFIRI KAMPASI YA PEMBA
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimezindua basi jipya aina ya TATA lenye uwezo wa kubeba abiria 41 kwa ajili ya kusafirisha watumishi na wanafunzi wa Kampasi ya Pemba, hatua inayolenga kuboresha huduma za usafiri chuoni hapo. Akizindua basi hilo, Mkuu wa Chuo, Prof. Haruni Mapesa, amewataka watumishi na wanafunzi kulitunza na kulitumia kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa ili liweze kudumu na kutimiza malengo yaliyokusudiwa. Prof. Mapesa amesema chuo kinaendelea kuwekeza katika miundombinu na huduma za usafiri kama sehemu ya juhudi ... za kuboresha mazingira ya kazi na kujifunzia, pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Naye Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Rose Mbwete, amepongeza hatua hiyo, kuwa itarahisisha utekelezaji wa shughuli za kitaaluma na kuimarisha maendeleo ya kampasi hiyo. Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Evaristo Haulle, amesema chuo kimejipanga kuhakikisha basi hilo linasimamiwa na kutumika ipasavyo kwa manufaa ya watumishi na wanafunzi wa Kampasi ya Pemba. Kwa upande wake, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Samir Nasir amekipongeza chuo kwa kuzingatia mahitaji ya usafiri wa wanafunzi wa Kampasi ya Pemba, akisema hatua hiyo itasaidia kurahisisha shughuli zao na kuimarisha mazingira ya kujifunzia. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 26.10.26 Read more →