Latest News

PROF. MAPESA AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA KAMAPSI YA PEMBA

Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Prof. Haruni Mapesa, amekutana na kuzungumza na Wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na Wanafunzi wanaoendelea na masomo kwa mwaka wa masomo 2026/2027 katika kampasi ya Pemba, Pujin Zanzibar. Akizungumza na Wanafunzi hao, Prof. Mapesa ameeleza kuwa Chuo kinaendelea na juhudi za kuboresha Miundombinu na Mazingira ya Kujifunzia na Kufundishia ili kuwawezesha Wanafunzi kupata Elimu bora, kuhakikisha wanakuwa na Nidhamu wakati wote wanapokuwa Chuoni. Mkuu huyo wa Chuo amewataka Wanafunzi k ... ufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Chuo pamoja na kuwa Waadilifu, kuheshimiana na kujali wengine. Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma,Utafiti na Ushauri wa kitaaluma, Prof. Rose Mbwete amewakaribisha Wanafunzi hao na amewataka wae Mabalozi wazuri wa MNMA kwa kuonesha Nidhamu, Maadili mema na kukitangaza vyema Chuo ndani na nje ya Taasisi. Naye, Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Evaristo Haulle ameeleza kuwa Chuo kinaendelea na jitihada za kuongeza idadi ya Wafanyakazi katika Kampasi ya Pemba ili kukidhi mahitaji ya huduma zinazohitaji. Aidha, amebainisha juhudi zinazofanywa na Taasisi katika kuendelea kuboresha eneo la Usafiri katika Kampasi hiyo. Kupitia kikoa hicho, Wanafunzi walipata fursa ya kuuliza Maswali, kutoa Maoni na kuainisha changamoto mbalimbali, ambazo baadhi zilijadiliwa kupatiwa majibu na nyingine zilipokelwa kwa hatua ya kufanyiwa kazi. Imetolewa na; Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 10.11.2026 Read more →