Latest News

WAHITIMU MNMA WAASWA KUWA WAZALENDO NA MABALOZI WEMA WA CHUO

Wahitimu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), wametakiwa kuwa wazalendo, Waadilifu wahakikishe wanakuwa Mabalozi wazuri wa kukitangaza chuo, pia waendelee kuwasilisha mawazo, na maoni chanya ya namna bora ya kuboresha huduma zinazotolewa chuoni. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo hicho Prof. Haruni Mapesa alipokuwa akizungumza katika kusanyiko la Baraza la Wahitimu wa chuo lililofanyika katika kampasi ya Kivukoni jijini Dar es salaam ambapo alisisitiza kuwa utendaji kazi bora na Maadili ya Wahitimu katika maeneo yao ya Ajira n ... diyo chachu itakayokifanya Chuo kiendelee kuheshimika. Mkuu huyo wa Chuo ameitaka Ofisi ya Mratibu wa Kusanyiko la Baraza la Wahitimu kuongeza kasi ya kuhamasisha wahitimu kujisajili pamoja na kukamilisha Katiba ya baraza itakayokuwa mwongozo wa utendaji kazi wa baraza hilo la Wahitimu. Kwa upande wake, Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Rose Mbwete amesema kusanyiko hilo ni muhimu katika kujenga mtandao imara wa mashirikiano, kukuza taswira ya chuo, kutoa ushauri na kuwa Viongozi wa Kongamano hilo ni kiunganishi kati ya Uongozi wa Chuo na Wahitimu kwa lengo la kufikia Maendeleo yanayokusudiwa na Chuo. Naye Katibu wa Baraza la Wahitimu Jumanne Muruga ameishukuru Menejimenti ya Chuo kwa kukubali kushughulikia maombi mbalimbali yanayolenga kuboresha utendaji kazi wa baraza hilo la Wahitimu, ikiwemo kupatikana kwa Mratibu na ofisi kwa ajili ya kuratibu shughuli za baraza la Wahitimu. Mada kuu iliyojadiliwa katika Kusanyiko hilo la Wahitimu ni KUTOKA KUTAFUTA AJIRA HADI KUZALISHA FURSA, ambapo wahitimu walijadili, walitoa maoni na kutunukiwa vyeti kwa Wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma, pamoja na viongozi wa Serikali ya Wanafunzi (MASO) ambao wamemaliza muda wao 2025/2026. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko. Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 19.11.2026 Read more →