MHE. WASIRA AWATAKA WAHITIMU WASIBWETEKE NA BADALA YAKE WAJIENDELEZE KWA MASLAHI YA TAIFA
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mhe. Stephen Wasira amewataka Wahitimu wa Chuo hicho kuhakikisha wanajiendeleza kitaaluma na wasiridhike na Elimu waliyoipata Chuoni hapo kwa Maslahi yao binafsi na ustawi wa Taifa kwa ujumla. Mhe. Wasira amesema hayo wakati wa Mahafali ya 21 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika kampasi ya Kivukoni jijini Dar es salaam ambapo amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi wema na raia wa mfano katika jamii zinazowazunguka. Aidha Kiongozi huyo, ameipongeza Menejimenti ya chuo kwa kufanikisha ... Mahafali, lakini pia amepongeza juhudi za Uhuishaji na Uendeshaji wa Mitaala Katika programu hizo 16 ambazo zitaanza kutolewa katika mwakaka wa masomo 2026/2027 na kuwa hatua hiyo ni ya kujivunia sana na kuwa inaongeza fursa na wigo kwa watanzania wengi kupata Elimu. Mhe. Wasira amekitaka Chuo hicho kujipanua zaidi katika Shahada za Umahiri na baadae Programu za Shahada za Uzamivu na kuhakikisha program hizo zinakidhi mahitaji ya soko kwa Wahitimu kuweza kujiajiri na kuajiriwa. Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho Prof. Haruni Mapesa ametaja Malengo sita ya Chuo hicho ikiwa ni pamoja na , kutoa Mafunzo katika fani mbalimbali kwa kiwango cha Stashahada, Astashahada, Shahada na Shahada za Umahiri, kufanya utafiti katika nyanja Mbalimbali ili kusaidia kutatua changamoto katika jamii, kutoa ushauri wa Kitaalamu katika Sekta ya Umma na Sekta binafsi na kuendesha Mafunzo ya Elimu ya kujiendeleza, kuendesha Mafunzo ya muda mfupi ya Uongozi na Utawala, Lugha ya Kichina, Kiswahili kwa wageni na Chuo kutumika kama kituo cha kufanyia mitihani ya lugha mbalimbali. Prof. Mapesa ameishukury Serikali kupitia bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu kwa kuendelea kutoa mikopo na hivyo kuwezesha Vijana wengi Kusoma. Mkuu huyo wa Chuo alisema Zaidi ya Wahitimu Elfu Nne wamehitimu Mafunzo yao kwa mwaka wa masomo 2025/2026 ambapo kati yao Wanawake ni 2,504 sawa na asilimi 52 na Wanaume 2,243 sawa na asilimia 48. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 20.11.2026 Read more →