Latest News

WASIRA AWATAKA WAHITIMU KAMPASI YA PEMBA KUJIENDELEZA KIELIMU

Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mhe. Stephen Wasira amewataka Wahitimu kuendelea kusoma zaidi na kuwa Elimu waliyoipata Chuoni hapo ni msingi tu, Pia amewataka wahakikishe wanakuwa Mabalozi wazuri wa Chuo hicho. Mhe. Wasira ameyasema hayo wakati wa Mahafali ya 4 Kampasi ya Pemba, ambapo amewasisitiza Wahitimu kuendelea kuwa Wadilifu, Wazalendo na kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kuwa raia wema katika Taifa. Kiongozi huyo amesema Elimu ina kazi moja tu, ambayo ni kuleta mabadiliko katika eneo ambalo mtu ... mnaishi, hakikisheni mnaleta mabadiliko kwenye Jamii mnazoishi kwani mtu aliyesoma na ambaye hajasona hawawezi kuwa sawa, nendeni mkalete mabadiliko. Awali akimkaribisha mgeni Mkuu wa Chuo hicho,Prof. Haruni Mapesa amewasihi wahitimu kuyachukulia mahafali hayo kama mwanzo wa safari mpya ya kielimu na si mwisho wa kujifunza. Mapesa amewahimiza kuendelea kuongeza maarifa na kutumia ujuzi walioupata chuoni katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuchangia maendeleo ya jamii wanazooshi. Naye mwanafunzi aliyefanya vizuri katika Taaluma Katika Kampasi hiyo , Suleiman Omari Mohamed, amesema wahitimu wote, ametoa shukrani kwa Serikali, uongozi wa Chuo, walimu, walezi na familia kwa mchango wao katika kufanikisha safari yao ya elimu mpaka kuhitimu Ameeleza kuwa mafanikio waliyoyapata yametokana na kujituma, kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano mzuri kati ya wanafunzi na walimu, hivyo ameishukuru Serikali kwa kutoa mikopo ya elimu ya juu iliyowawezesha wanafunzi kupata fursa ya kuendelea na masomo yao. Read more →