CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHAADHIMISHA MIAKA 100 TANGU KUZALIWA BABA WA TAIFA LA TANZANIA
Waziri wa Elimu, Sayanai na Teknolonia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema Hayati baba wa Taifa Malimu Julius K. Nyerere anakumbukwa kwa sababu ya maono yake, falsafa zake ikiwemo ile ya kuamini binadamu wote ni sawa na kuwa dhana hiyo ni ya muda mrefu na imelenga kutetea usawa wa kijinsia. Prof Mkenda amesema hayo leo katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Kivukoni jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la kuadhimisha miaka mia moja tangu kuzaliwa baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Profesa Mkenda amesema, kwa sa ... a dhana ya binadamu wote ni sawa inaweza isionekane ina umuhimu sana, lakini andiko la kwanza la baba wa Taifa lilihusu kutetea usawa wa kijinsia na kutetea haki za wanawake lengo lake kuu lilikuwa ni akitetetea haki za binadamu. Prof Mkenda alisema Baba wa Taifa hakuingia kwenye siasa kwa ajili ya kutafuta madaraka badala yake alitaka usawa kwa binadamu wote, ikiwa ni pamoja na kupigania maslahi ya wananchi wote. Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo Prof Shadrack Mwakalila amesema dira ya chuo hicho ni kuwa kitovu cha utoaji wa maarifa bora kwa kutoa elimu na mafunzo kuhusu ubunifu na uvumbuzi sambamba na kuendeleza amani na umoja wa kitaifa Prof. Mwakalila amesema tayari zoezi la kuandaa mitaala mipya na kuhuisha ya zamani limekamilika ili kuwa na mitaala inayozingatia mahitaji halisi ya kitaifa na kimataifa na kwamba katika maboresho hayo somo la Uongozi,Maadili na uzalendo limeingizwa katika mitaala yote ili kila mwanafunzi awe na ufahamu wa kutosha kuhusu maadili uzalendo na uongozi Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Stephen Wassira akizungumza wakati wa kongamano hilo alimtaja Mwalimu J. K. Nyerere kuwa ndiye muasisi wa misingi ya Amani, Umoja na Mshikamano, na kuwa wakati wa utawala wake hakujali dini, kabila wala utaifa na badala yake aliamini umoja na mshikamano. Mada kuu katika kongamano hilo ni Misingi ya Urithi wa Mwalimu Julius Nyerere katika kujenga Amani, Umoja na Maendeleo ndani na nje ya Afrika. Imetolewa na; Kitengo cha Habari na Mawasiliano CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 4.4.2022 Read more >
[ 2022-06-07 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam