|
|
RAIS DKT. MWINYI AMEKIPONGEZA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWL. NYERERE KWA KUENDESHA KONGAMANO LA KARUME
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema nchi itaendelea kuenzi falsafa, maono na dhamira ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ili kuendelea kuacha urithi bora kwa vijana wetu.
Akizungumza wakati akifungua kongamano la Nne la Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza Mapainduzi la Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume Rais Dkt Mwinyi amesema ni vyema Makongamano ya namna hii yakatumika vizuri kwa vijana wetu kujifunza yale yaluyoasisiwa na viongozi wetu.
"Nakipongeza sana Chuo cha Kumbukumb ...
ya Mwalimu Nyerere kwa kuandaa kongamano la namna hii ambapo pia limeshirikisha makundi mbalimbali ikiwemo vijana, vyama vya siasa, wazee, na viongozi wastaafu kwa lengo la kujifunza maono ya Waasiai wetu, hili ni jambo jema na pia linatakiwa liigwe,"alisisitiza Dkt. Mwinyi.
Dkt Mwinyi amesema Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimekuwa ni kielelezo cha kuendelea kuenzi Falsasa, kuhamasisha umoja wa Taifa letu na hivyo ipo haja ya kuendelea kuhamasisha makongamano ya namna hii.
Akizungumza katika kongamano hilo Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila ameishukuru serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano ambao Chuo kinapata na hivyo kusaidia kufikia malengo ambayo imejiwekea.
Prof. Mwakalila amesema Chuo kimekuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi kutoka wanafunzi ishirini na mbili hadi kufikia wanafunzi zaidi ya elfu mbili kwa kampasi ya Karume- Zanzibar pamoja na kuongezeka kwa idadi ya kozi mbalimbali.
Profesa Mwakalila amesema Ujenzi kwa ajili ya hosteli za Kampasi unaendelea na utakamilika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu ambapo utagharinu kiasi cha Shilingi bilioni 15.2.
Amesema tayari zoezi la kuandaa mitaala mipya na kuhuisha ya zamani limekamilika ili kuwa na mitaala inayozingatia mahitaji halisi ya kitaifa na kimataifa na kwamba katika maboresho hayo somo la Uongozi,Maadili na uzalendo limeingizwa katika mitaala yote ili kila mwanafunzi awe na ufahamu wa kutosha kuhusu Uongozi, Maadili na Uzalendo.
Akizungumza katika Kongamano hilo Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Mzee Stephen Wasira amesema huwezi kundika historia ya Tanzania au Zanzibar bila kumtaja Hayati Mwalimu Jullius Kambarge Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume
Awali akitoa utambulisho wa wageni waalikwa katika kongamano hilo Mkuu wa Kampasi ya Karume Dkt. Rose Mbwete amesema Lengo la kongamano hilo ni kuwaleta wananchi pamoja kwa ajili ya kujadili na kujifunza falsasa za Waasisi wa Taifa.
Kauli mbiu katika Kongamano hilo ni "Mchango wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume Katika Maendeleo ya Elimu na Uchumi wa Zanzibar."
Read more >
[ 2022-06-07 ]
|
|
|
|