|
|
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHAINGIA KUMI BORA YA WABUNIFU MAKISATU
Mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Hapsa Ahmed Gharib amebuni mfumo wa kufunga na kufungua maji kwa kutumia kadi.
Hapsa amesema mfumo huo unamruhusu mtumiaji kupata huduma wakati wowote endapo atakuwa amelipia kadi yake
Pia mfumo huo utaruhusu watumiani wengi kupata huduma kwa wakati mmoja kwa sababu kila mtumiaji atakachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kadi yake imelipiwa.
" Mita inaweza kukaa kwenye mtaa moja, kisha kila mmoja kwa wakati wake akaenda na kadi yake ikiwa imelipiwa kwa ajili ya huduma ya maji," anaema Ha ...
sa
Hapsa anasema mifumo ambayo imezoeleka ni ile ya kuwa na mita za maji majumbani, lakini mfumo huu wa kadi utamsaidia mteja kujihudumia mwenyewe kwa kuweka fedha kwenye kadi na kisha kupata huduma ya maji.
Lengo la Ubunifu huo ni kwenda kuondoa changamoto ya utumiaji wa mita zile ambazo zinamlazimu mtumishi wa idara ya maji kupita majunbani ili kubaini gharama ya maji iliyotumika na kisha kumkadiria malipo muhusika.
Kutokana na umuhimu wa ubunifu huo kwa jamii tayari Hapsa Ahmed Gharib ameingia kwenye kinyang'anyiro cha Kumi bora ( Top Ten).
Ili kuona Ubunifu wa Mwanafunzi huyo wa MNMA Hapsa Ahmed Gharib tembelea maonesho ya MAKISATU yanayofanyika mkoani Dodoma.
Imetolewa na :
Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
18.05.2022
Read more >
[ 2022-06-08 ]
|
|
|
|