KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU AKAGUA UJENZI UNAONDELEA WA JENGO LA MAKTABA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Maiko amekipongeza Chuo kwa jitihada mbalimbali ambazo imekuwa ikizifanya ikiwemo kuboresha Miundombinu ya Kujifunzia na kufundishia, pamoja na Wanafunzi kuibua bunifu ambazo zinalenga kutatua changamoto mbalimbali katika jamii. Dkt. Maiko amesema hayo leo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho ambapo alikutana na Menejimenti na Wakuu wa idara mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha lakini pia alikagua Miundombinu iliyopo pamoja na kukagua ujenzi unaoendelea wa j ... ngo la Maktaba lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2500, pamoja na kumbi za Mihadahara . Dkt. Maiko amesema lengo la ziara yake ni kuona namna atakavyoshirikiana na uongozi wa Chuo katika kutatua changamoto mbalimbali. " Mimi ni Mtumishi wenu, niko hapa kwa ajili ya kuwatumikia milango ya ofisi yangu iko wazi muda wowote na wakati wowote, tuwasiliane kwa lengo la kufanikisha yale yote ambayo Taasisi imejiwekea katika kutimiza malengo yake," alisisitiza Dkt. Francis Maiko. Awali akimkaribisha Katibu Mkuu, Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila pamoja na mambo mengine alimweleza Katibu Mkuu kuwa dira ya Chuo ni kuwa kitovu cha Utoaji wa Maarifa bora na katika kutekeleza hilo tayari Chuo kimehuisha Sera ya Uthibiti ubora, Mitaala pia imehuishwa kwa kuongeza kozi mbalimbali ikiwemo kozi ya Uongozi, Maadili na Utawala. Prof. Mwakalila alitaja baadhi ya mafanikio ya Chuo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa kozi zinazotolewa Chuoni hapo ambapo kwa sasa Kuna kozi zaidi ya 30. Kuwepo kwa ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa jengo la Maktaba na kumbi za mihadhara kwa kampasi ya kivukoni ambapo hadi kukamilika kwake itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 14 na ujenzi wa hosteli za Wanafunzi ambao unaendelea kwa kampasi ya Karume. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mahusiano CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 27.07.2022 Read more >
[ 2022-07-27 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam