|
|
PROF MWAKALILA AMEWATAKA WATENDAJI WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KUONGEZA TIJA KATIKA UTENDAJI KAZI
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema dira ya Chuo ni kuwa kitovu cha kutoa maarifa bora, na kuendeleza amani ya kitaifa.
Prof. Mwakalila ameyasema hayo leo wakati akifungua kikao cha Uchaguzi wa wajumbe wa baraza la Wafanyakazi na kusisitiza kuwa Jukumu kubwa la Taasisi hiyo ni Kutoa mafunzo, kutoa mafunzo ya Uongozi, Maadili, Utawala na Uzalendo, Kufanya tafiti mbalimbali zinazoenda kutatua changamoto katika jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu katika sekta zote.
Hivyo amewataka Wajumbe wa Baraz ...
la Wafanyakazi kutambua majukumu ya Msingi ya Taasisi hiyo pamoja na kuhakikisha tija inaongezeka katika utendaji kazi.
Mkuu huyo wa Chuo ameeleza kuwa Wajibu na Haki vinaenda pamoja hivyo Mfanyakazi ana wajibu wa kutimiza majukumu yake ipasavyo, lakini pia mfanyakazi ana haki.
"Mfanyakazi anapodai haki zake basi ahakikishe ametimiza wajibu wake, kama wewe ni Mwanataaluma basi tumia uwezo wako kufanya vizuri, na kama wewe ni mwendeshaji basi hakikisha unatimiza majukumu yako ipasavyo kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sharia,”alisisitiza Prof.Mwakalila.
Uchaguzi huo umefanyika baada ya Wajumbe waliokuwa wanatumikia nafasi hizo kumaliza muda wao.
Uchaguzi huo umesimamiwa na Afisa Mwanadamizi kutoka ofisi ya kamishana wa Kazi, pamoja na viongozi wa wafanyakazi kutoka RAAWU na THTU.
Inetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mahusiano
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
13,10.2022
Read more >
[ 2022-10-14 ]
|
|
|
|