|
|
DKT. FRANCIS MICHAEL AMEKIPONGEZA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWA KUSIMAMIA MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi ja Teknolojia Dkt. Francis Michael amepongeza Menejinent, bodi ya Chuo na wafanyakazi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa uwajibikaji na hivyo kukifanya Chuo kuzidi kupiga hatua za kimaendeleo.
Dkt. Francis ameyasema hayo leo katika Mahafali ya Saba ya Kampasi ya Karume ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Zanzibar.
Dkt. Francis amesema Chuo kimejikita zaidi katika kutoa Mafunzo ya Uongozi na Maadili na hivyo amewataka Watumishi, Wahitimu kuonyesha mifano zaidi katika Maadi ...
i ili kuendelea kukijengea sifa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Amesema Serikali ya awamu ya Sita imejipanga vyema kuhakikisha Chuo kinafikia malengo iliyojiwekea,huku akiwataka Wahitimu kuendelea kubeba taswira na Sifa ambazo Chuo imekuwa nacho.
Amewapongeza Wazazi na Walezi kwa kuendelea kukiamini Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kutokana na msingi ambayo Chuo imekuwa ikisimamia tangu kuanzishwa kwake.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila amesisitiza kuwa dhima ya Chuo ni kujitolea kwa dhati kuendeleza utoaji wa Elimu ya Kudumu kupitia Ufundishaji bora,utafiti, kuwa na Mazingira ya kujifunzia yanayosaidia upataji wa Maafira,Utafiti wa Ubunifu, umakini na Stadi tumizi zitaendelezwa na kudumishwa.
Profesa Mwakalila amebainisha kuwa wahitimu zaidi ya Elfu Moja na Mia Tano wanetunukiwa vyeti, ambapo kati yao wanawake ni asilimia 61 na Wanaume ni asilimia 39.
Katika Mahafali hayo ya Saba Wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo kwa kampasi ya Karume na Pemba walitunukiwa vyeti na fedha, huku Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi ambao wamemaliza muda wao nao wakitunukiwa vyeti.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mahusiano
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
28.11.2022
Read more >
[ 2022-12-01 ]
|
|
|
|