|
|
MKUTANO MAALUMU WA SACCOS YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE WAFANYIKA LEO
Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni ( KIVUKONI SACCOS LTD) leo kimefanya Mkutano Mkuu Maalumu wa Kumkaribisha mlezi wa Chama hicho ambaye ni Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo kwenye mkutano huo Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Fedha na Mipango Bi. Ukende Mkumbo amewataka Wananchama wa Chama hicho kujiimarisha katika kusimamia Chama na kuhakikisha wanachama waliokopa wanarejesha mikopo.
Bi Ukende amesema dhamana ya kurejesha mkopo ni ...
a Mwanachama husika, lakini dhamana ya kusimamia Chama ni ya Wanachama wote.
Wanachama wametakiwa kuzingatia taratibu na Sheria za kukopa ili kuepusha usumbufu miongoni mwa Wanachama.
Kupitia Mkutano huo Maalumu wa Wanachama wa KIVUKONI SACCOS LTD walipitisha Sera, Miongozo na Kanuni mbalimbali za namna ya Mwanachama anavyoweza kupata mkopo wa Nipige Tafu, Mkopo wa Sikukuu, Mkopo Mdogo,Mkopo wa dharura na Mkopo wa Maendeleo.
Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI NA MASOKO
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
10.01.2023
Read more >
[ 2023-01-11 ]
|
|
|
|