|
|
BARAZA LA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE LAPITISHA MAOTEO YA BAJETI YA MWAKA 2023/2024
Baraza la Wafanyakazi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo limepokea na kujadili taarifa ya Maoteo ya Bajeti ya Chuo kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo kwa kauli moja wamepitisha maoteo ya bajeti hiyo.
Akizungumza na Wajumbe wa baraza hilo katika mkutano Maalumu wa kwanza wa Baraza la Wafanyakazi Mkuu wa Chuo hicho Prof. Shadrack Mwakalila amesema suala la bajeti ni mchakato ambao unaanzia ngazi ya idara hadi kuwasilishwa Wizarani na hatimae bungeni.
Katika taarifa iliyowasilishwa kwa wajumbe wa Mkutano wa baraza hilo imeanisha ...
vipaumbele vya Chuo kwa mwaka 2023/24 ikiwa ni pamoja na kuendelea na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo, kufanya ukarabati wa Miundombinu ya Majitaka, Umeme, barabara ,Majengo na kuajiri Wafanyakazi Wapya 95 ili kuboresha Utoaji huduma.
Taarifa hiyo imeainisha vipaumbele vingine ni Kuwezesha Shughuli za Utafungwa na Ushauri wa Kitaalamu, kuendelea kugharamia mafunzo ya kuinua ujuzi kwa Wafanyakazi Wanataaluna na Waendeshaji, kutunga na kupitia mitaala ya Chuo ili iweze kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri, Kuboresha na kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika kuendesha shughuli mbalimbali za Chuo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Masoko
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
11.01.2023
Read more >
[ 2023-01-12 ]
|
|
|
|