|
|
PROF. MWAKALILA AMEWATAKA WANAFUNZI WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KUSOMA KWA BIDII NA KULIPA ADA KWA WAKATI
Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila leo amezungunza na Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa masomo kwa mwaka 2022/20223 ambapo amewaasa wanafunzi hao kuzingatia zaidi masomo ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii, juhudi na maarifa .
Profesa Mwakalila amewataka Wanafunzi hao kuwa Waadilifu ,Waminifu na kuzingatia suala la ulipaji ada kwa wakati.
"Suala la kulipa ada ni la muhimu sana,kabla ya kuja hapa Chuoni kila mmoja alijipanga kuja kusoma, hili siyo jambo la dharura na ilikuwa ni mipango ya muda mref ...
hivyo ni wajibu ada ilipwe kwa wakati,"alisistiza Profesa Mwakalila.
Mkuu huyo wa Chuo amewataka pia Wanafunzi hao kujiepusha na udanganyifu wa aina yoyote pindi Mwanafunzi anapokuwa chuoni, kujiepusha na mambo ambayo hayawezi kumsaidia katika masomo, kujiepusha na migogoro yoyote au makundi ya uchochezi na sula zima la kuheshimiana kati ya Walimu na Wanafunzi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
25.01.2023
Read more >
[ 2023-01-25 ]
|
|
|
|