UONGOZI WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE WAWAPONGEZA WANAFUNZI KWA USHINDI
UONGOZI wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) umewapongeza wanafunzi wanamichezo wa chuo hicho walioshiriki kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vya Elimu ya Juu Tanzania (SHIMIVUTA) kwa kukiheshimisha chuo na kurejea na kombe la ushindi wa kwanza kitaifa kwenye mchezo wa mpira wa kikapu (Basket Ball)
Akizungumza jkwenye hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi wanamichezo walioshiriki Mashindano ya SHIMIVUTA yaliyomalizika hivi karibuni Jijini Mwanza Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa kitaalamu Prof Ric ...
ard Kangalawe kwa niaba ya Mkuu wa chuo Prof Shadrack Mwakalila aliahidi kuendelea kuwawezesha wanafunzi kwa kuwapatia fursa ya kushiriki mashindano mbalimbali.
Alisema ushindi wa kwanza kitaifa kwenye mchezo wa kikapu ni kitu Cha kujivunia na hii itaendelea kuhamasisha wachezaji kujituma zaidi katika Mashindano mengine.
Aidha aliitaja ushindi mwingine ulioletwa na wanamichezo hao kuwa ni pamoja na medali nane kwa wanariadha na michezo mbalimbali
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Dkt.Evaristo Haulle alisema pamoja na kwamba michezo ni afya lakini ushindi huu umekiheshimisha chuo na kukitangaza.
Aliwataka wanafunzi kutambua namna uongozi unavyowathamini na kuendelea kukua kwenye misingi mema ya maadili kwani ndiyo azma kuu ya Chuo.
Hata hivyo baadhi ya Wanafunzi walioshiriki michezo walisema wamefarijika kwa namna chuo kilivyowathamini na kutambua mchango wao na kuahidi ushirikiano wa kutosha kwenye Mashindano yajayo huku wakisisitiza wanawake kujitokeza zaidi.
Inetolewa na:
Kitengo cha Habari na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
26.01.2023
Read more >
[ 2023-01-27 ]