|
|
MWILI WA DKT. NTIDE PIUS DADI WA MNMA WAAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
Uongozi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo umeungana na Wafanyakazi wa Chuo hicho katika kumuaga aliyekuwa mtumishi wa Chuo hicho Dkt Ntide Pius Dadi aliyefariki wakati akiwa mazoezini nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika salamu za Pole wakati mwili wa marehemu ukiwa kwenye kanisa la Waadventista Wasabato lililopo Segerea ijini Dar es Salaam Mkuu wa chuo Profesa Shadrack Mwakalila amesema wanadamu wote tunatakiwa kuwa na hofu ya Mungu kwa sababu hatujui kesho yetu na kuwa Mungu pekee ndiyo Mkuu.
Akisoma Wa ...
ifu wa Dkt. Ntide Pius Dadi Mkuu wa Kampasi ya Karume - Zanzibar Dkt. Rose Mbwete amesema Chuo kimempoteza mwanazuoni mahiri, familia na Taifa limepoteza hazina kubwa lakini yote ni mipango ya Mungu.
Mwili wa Dkt Ntide Dadi utasafirishwa kesho kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika mkoani Kigoma.
Chuo kinatoa pole kwa Watumishi, Familia, Ndugu na Jamaa.
Imetolewa na :
KITENGO CHA HABARI NA MASOKO
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
4.05.2023
Read more >
[ 2023-05-04 ]
|
|
|
|