PROF. MWAKALILA AMEWATAKA WATUMISHI WA MNMA KUZINGATIA DIRA NA MAJUKUMU YA CHUO PAMOJA NA TARATIBU ZA UTUMISHI WA UMMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amekutana na kuzungumza na Wafanyakazi kuhusu Masuala mbalimbali ya kiutumishi ambapo amewataka watumishi kutambua Dira ya Chuo kuwa ni kitovu cha utoaji wa Maarifa bora kwa kutoa Elimu na Mafunzo kuhusu ubunifu na Uvumbuzi na Kuendeleza Amani na Umoja wa Kitaifa. Profesa Mwakalila amesema hayo mwishoni mwa Wiki alipokutana na Kuzungumza na Watumishi Chuoni hapo ambapo amesema chuo kina majukumu yake ya msingi ambayo ni, Kutoa mafunzo katika fani mbalimbali za kitaaluma ... kuanzia Astashahada, Stashahada, Shahada na shahada ya uzamili, Kutoa mafunzo ya Uongozi, Maadili, Uzalendo na Utawala bora; Kuendesha mafunzo ya Elimu ya Kujiendeleza, Kufanya tafiti zenye kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa sekta za umma na sekta binafsi. Prof. Mwakalila pia amebainisha kuwepo kwa ongezeko la idadi ya programu za Mafunzo ambapo kwa sasa zimefikia Programu 32. Programu hizo ni kwa ngazi ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma), Shahada za Awali na Shahada za Umahili.Katika Kampasi ya Kivukoni udahili umeogezeka kutoka wanafunzi 11,184 mwaka 2020/2021 hadi 11,939 mwaka 2022/2023, Aidha katika kampasi ya Karume – Zanzibar udahili umeongezeka kutoka 2,290, kwa mwaka 2021/2022 hadi 3530 kwa mwaka 2022/2023 na kampasi ya Pemba kwa mwaka 2022/2023 ina wanafunzi 228 ambapo jumla ya Wanafunzi kwa Chuo chote ni 14,457. Profesa Mwakalila amesema Chuo kimeongeza idadi ya wahitimu kwa Kampasi ya Kivukoni kutoka wanafunzi 4330 mwaka 2020/2021 hadi 5774 kwa mwaka 2021/2022, Aidha Katika kampasi ya karume – Zanzibar wahitimu wameongezeka kutoka Wanafunzi 1242 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Wanafunzi 3530 kwa mwaka 2021/2022 hivyo idadi ya wahitimu wote kwa mwaka 2021/2022 ni 9,304 . Amesema mafanikio mengine ni Chuo kimewezesha Wahadhiri 56 kwenda kwenye mafunzo kwa ngazi mbalimbali za masomo ikiwemo Shahada ya Uzamivu, Shahada ya Uzamili, Shahada ya Awali na Stashahada. Pia Chuo kimeongeza idadi ya Walimu/Wahadhiri wenye shahada ya uzamivu (PhD) katika Kampasi ya Kivukoni imeongezeka kutoka wahadhiri 40 kwa mwaka 2020 hadi wahadhiri 46 mwaka 2023. Amesema hadi kufikia Februari, 2023 Chuo kina jumla ya watumishi wa kudumu 307, ambapo kati yao watumishi wa Kampasi ya Kivukoni ni 228 , Kampasi ya Karume Zanzibar ni 60 na Kampasi ya pemba 19. Kati ya watumishi hao, jumla ya watumishi wanataaluma Chuoni ni 233 na watumishi wasio wanataaluma ni 74. Mkuu wa Chuo amesema, Chuo kimekuwa na bunifu nyingi lakini Jumla ya bunifu 22 zimeshindanishwa kwenye maonesho mbalimbali ambapo kati ya bunifu hizo bunifu Moja ya ilishika nafasi ya pili kitaifa katika mashindando ya maonesho ya Kitaifa ya Sayansi Tekinolojia na Ubunifu (MAKISATU) na Nyingine ilishika nafasi ya nne kitaifa katika Maonyesho hayo hayo kwa mwaka 2020/21. Mwaka 2022/23 Chuo kiliingia katika bunifu kumi bora. Kuhusu Michezo., Profesa amesema michezo imekuwa ni suala la kipaumbele ili kubore Read more >
[ 2023-05-31 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam