|
|
PROF. MWAKALILA AZUNGUMZA NA SERIKALI YA WANAFUNZI YA MNMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila leo amemwapisha Waziri Mkuu mpya wa Serikali ya Wanafunzi- MASO- Rashid Tibita.
Akizungumza na Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi ya Sasa na ile ambayo imemaliza muda wake, Prof. Mwakalila amesema dhamana ya kuongoza ni fursa ya kwenda mbele na siri ya kufanikiwa katika uongozi ni ushirikishwaji.
“Kipekee kabisa nichukue nafasi hii kupongeza uongozi wa serikali ya Wanafunzi Uliomaliza muda wake kwa kutimiza majukumu yake kwa Weledi, naamini hata Serikali hii mpya ...
mtafanya kazi zenu kwa Kufuata taratibu,Kanuni na Sheria za Taasisi.”Alisisitiza Prof. Mwakalila.
Mkuu Huyo wa Chuo amesema
Serikali ya Wanafunzi ni kiungo muhimu Katika utendaji wa shughuli za Chuo na ndiyo maana hata mafanikio ambayo yanaptikana Chuoni Serikali ya Wanafunzi imechangia na kuhusika moja kwa moja.
“ Mafanikio ya Chuo ambayo leo tunajivunia basi Serikali ya Wanafunzi na yenyewe ina mchango wake mkubwa.” Alisema Prof Mwakalila.
Mkuu huyo wa Chuo amemkabidhi Waziri Mkuu huyo mpya vitendea kazi ikiwemo, Katiba ya Serikali ya Wanafunzi, Sheria ndogondogo za Wanafunzi, na Prospectus.
Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
7.06.2023
Read more >
[ 2023-06-08 ]
|
|
|
|