|
|
PROFESA MWAKALILA ASISITIZA UADILIFU, UAMINIFU NA UZALENDO KWA VIONGOZI WA WANAFUNZI
Mkuu wa Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amewapongeza viongozi wapya wa serikali ya Wanafunzi (MASO) kwa kuaminiwa na Kuchaguliwa Kuwa viongozi kwa mwaka 2023/24 ambapo amewataka viongozi hao kutumia vizuri fursa hiyo.
Prof. Mwakalila amesema hayo leo wakati wa Semina elekezi ya kuwajengea uwezo viongozi wapya wa Serikali ya Wanafunzi huku akiwataka viongozi hao kuwa mfano wa kuigwa kwa kuhakikisha wanasoma kwa juhudi na Maarifa na kufanya vizuri katika Mitihani.
Mkuu huyo wa Chuo pia amewata Viongozi hao wa ...
Wanafunzi kuwa Waadilifu,Waaninifu na Wazalendo kwa Chuo na Taifa kwa ujumla, pamoja na kuhakikisha ada zinalipwa kwa wakati.
Prof. Mwakalila pia amewataka Viongozi hao wa Wanafunzi kujiepusha na udanganyifu wa aina yeyote katika Mitihani na kujiepusha na Makundi ya Uchochezi.
" Nasisitiza suala la kuheshimu Wafanyakazi wote, Walimu na Waendeshaji lakini Muwaheshimu na Wanafunzi wenzenu pia,"alisiaitiza Prof. Mwakalila.
Amewataka Wanafunzi kuhakikisha wanatumia vizuri mitandao ya kijamii kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya kimasomo na si vinginevyo.
Imetolewa na;
Kitengo Cha Habari na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
19.06.2023
Read more >
[ 2023-06-20 ]
|
|
|
|