|
|
PROFESA MWAKALILA AWAASA WAZAZI KUHUSU WATOTO WAO KUJIUNGA NA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Mkuu wa chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amewaasa wazazi kuhakkisha watoto wao wanajiunga na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuwa Chuo hicho kinatoa Elimu yenye kukuza vipaji vya Wanafunzi na Kuwajengea uwezo katika kuandaa bunifu kulingana na taaluma mbalimbali.
Prof. Mwakalila ameyasema hayo baada ya kutembelea Banda la Chuo katika Maonesho ya wiki ya Elimu ya Juu yanayofanyika katika kamapasi ya Pemba,iliyopo ChakeChake Pemba.
Akiwa katika Maonesho hayo Prof. Mwakalila ambaye aliambatana na Vi ...
ngozi mbalimbali wa kampasi hiyo alijionea mfumo wa TEHAMA uliobuniwa na Mwanafunzi kutoka Kampasi ya Pemba Mansour Juma Khamis, Mfumo wenye uwezo wa kutuma taarifa zote muhimu za Mwanafunzi kwa Mzazi, ikiwemo mahudhurio ya Mwanafunzi husika.
Aidha, Prof. Mwakalila ameupongeza Uongozi wa Kampasi na wanafunzi kwa kushiriki vyema katika maonyesho hayo ya Wiki ya Elimu ya Juu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
31.08.2023
Read more >
[ 2023-09-01 ]
|
|
|
|