KUSANYIKO LA WAHITIMU MNMA LAFANYIKA, MKUU WA CHUO AELEZEA MAFANIKIO YA CHUO HICHO
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila leo amezungumza na Wahitimu mbalimbali wa Chuo hicho wakati wa Kusanyiko la Wahitimu –CONVOCATION – na kueleza kuwa Dira ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni kuwa kitovu cha utoaji wa maarifa bora kwa kutoa Elimu na Mafunzo kuhusu ubunifu na uvumbuzi na kuendeleza Amani na Umoja wa Kitaifa. Profesa Mwakalila amesema Katika kuhakikisha Chuo kinafikia dira iliyojiwekea, Chuo kinatekeleza pamoja na mambo mengine majukumu makuu matano ambayo ni Kutoa mafunzo ka ... ika fani mbalimbali za kitaaluma kwa kiwango cha Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili; Kutoa mafunzo ya Uongozi, Maadili na Uzalendo; Kufanya tafiti zenye kutatua changamoto mbalimbali za kijamii; Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa sekta ya umma na sekta binafsi; na Kuendesha mafunzo ya Elimu ya Kujiendeleza. Amesema Katika mwaka wa fedha 2022-2023 Uongozi wa Chuo kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau mbalimbali umefanya jitihada mbalimbali za kutekeleza mipango yake ili kuwezesha Chuo kuwahudumia wadau mbalimbali kwa mafunzo, utafiti na ushauri wa kitaalamu. Pia Chuo kimepata mafanikio katika kuboresha Miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika kampasi zake zote tatu ikiwemo ya Kampasi ya Kivukoni, Karume na ile ya Pemba. Taarifa yake pia imeanisha kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo litakalo kuwa na Ukumbi wa Mihadhara wenye uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 1000 pamoja na Maktaba itakayo kuwa na uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 2500 kwa wakati mmoja unaendelea vizuri. Maboresho ya Miundombinu ya Kampasi ya Karume Miundombinu mbalimbali ya kufundishia na kujifunzia katika Kampasi ya Karume imeboreshwa ili kuongeza ubora wa mafunzo. Profesa Mwakalila amesema Vifaa mbalimbali vya kufundishia katika kumbi za mihadhara vimefungwa ikiwa ni pamoja na kufunga projector,Miundombinu ya madarasa katika Kampasi ya Karume Zanzibar, ina uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 5000 lakini wanafunzi waliopo ni chini ya 3000 kwa sababu ya ukosefu wa mabweni ya kulala wanafunzi. Hivyo, Chuo kinaendelea na ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1536 kwa wakati mmoja. Aidha ujenzi huu ukikamilika utawezesha kuongeza udahili wa wanafunzi ili kufikia wanafunzi 5000. Akizungumzia eneo la udahili Profesa Mwakalila amesema Udahili wa Wanafunzi katika Kampasi zote Kivukoni udahili umeogezeka kutoka wanafunzi 14,238 mwaka 2022/2023 hadi 14,457 mwaka 2023/2024. Kampasi ya Karume udahili uliongezeka kutoka wanafunzi 2,290 mwaka 2022/2023 hadi 2,400 mwaka 2023/2024. Kampasi ya Pemba udahili uliongezeka kutoka wanafunzi 151 mwaka 2021/2022 hadi wanafunzi 228 mwaka 2022/2023. Hivyo jumla ya Wanafunzi waliodahiliwa mwaka 2023/2024 ni 17,200. Ongezeko la wanafunzi ni ishara kuwa wanafunzi na wazazi wana imani na Chuo hiki na mategemeo makubwa ya kupata wahitimu walioelimika na wenye maarifa na ujuzi wa kuchangia kwa haraka Maendeleo yao na Taifa kwa ujumla. Amesema idadi ya Wahitimu imeongez Read more >
[ 2023-11-29 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam