|
|
PROF. MWAKALILA AWATAKA WANAFUNZI KUZINGATIA MALENGO YALIYOWALETA CHUONI
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amewataka wanafunzi waliopo chuoni hapo kuzingatia malengo yaliyowaleta chuoni na kujiepusha na makundi yasiyokuwa na tija.
Prof. Mwakalila ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Karume -Zanzibar ambapo amesema kuwa pamoja na taaluma nyingine ambazo zipo chuoni hapo pia chuo kimejikita katika kuwajenga wanafunzi katika Maadili, Uzalendo na Utawala bora ili waweze kuwa raia wema kwa ustawi wao binafsi na ...
aifa kwa ujumla.
“ Tunategemea Mwanafunzi anayesoma Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere awe tofauti na Mwanafunzi wa Chuo kingine kwa kuwa hapa kuna kozi maalumu ya Masuala ya Uongozi, Maadili na Uzalendo ambayo yanawajengea uwezo katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika Jamii inayowazunguka,” Alisisitiza Prof. Mwakalila.
Profesa Mwakalila pia amewaasa Wanafunzi Kusoma kwa bidii na Maarifa ,kulipa ada kwa wakati na kuheshimu wafanyakazi katika kipindi chote cha masomo wawapo chuoni hapo.
Aidha,Prof. Mwakalila aliwataka wafanyakazi kutambua kuwa wao ni walezi wa wanafunzi wawapo chuoni hapo na hivyo wahakikishe wanazingatia Kanuni,Sheria,Taratibu na Miongozo iliyopo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Chuo,
Mkurugenzi wa Kampasi ya Karume Dkt.Rose Mbwete amewataka Wanafunzi kutimiza wajibu wao wanapokuwa chuoni, huku akitilia mkazo kuwa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni sehemu sahihi na salama kitaaluma.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
7.12.2023
Read more >
[ 2023-12-07 ]
|
|
|
|