|
|
KONGAMANO LA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA LAFANYIKA MNMA
Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amesema Chuo kinatekeleza kwa vitendo katika kupinga ukatili wa kijinsia kwa kuwa na idara maalumu inayotoa mafunzo ya kijinsia kuanzia ngazi ya cheti hadi Shahada ya umahiri.
Prof. Kangalawe ameyasema hayo leo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila wakati akifungua kongamano la kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia lililofanyika Chuoni hapo.
Prof Kangalawe ambaye amemwakilisha Mkuu wa Chuo amesema kufanya vitendo Vya ukatili wa k ...
jinsia ni kukosa Maadili na kuwa vitendo hivyo vinatakiwa kupigwa vita.
Amesema Chuo kinaunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa mafunzo ya Uongozi na Maadili, na katika kila moduli wanafunzi wanafundishwa Uongozi, uzalendo, Maadili na Utu lengo Ni kuwaandaa vijana wenye Maadili na Uzalendo.
Awali akizungumza na washiriki Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Fedha na Mipango Dkt Evaristo Haule amesema kongamano hilo ni sehemu ya kutukumbusha na kufanya tafakuri tumepiga hatua gani katika kupinga ukatili wa kijinsia.
Lengo kuu ni kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokomezwa,na kuwa sisi sote ni ndugu,katika kutekeleza hili Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imetenga dawati la jinsia kwa lengo la kuhakikisha usawa wa kijinsia unapatikana.
Kwa upande wake Mratibu wa dawati la kijinsia Dkt. Patricia Mwesiga amesema jamii bado inahitaji kuelimishwa katika kupambanua matendo ya ukatili wa kijinsia.
Mada mbalimbali zimejadiliwa katika kongamano hilo la siku moja.
Kauli mbiu:Wekeza kuzuia ukatili wa Kijinsia.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
8.12.2023
Read more >
[ 2023-12-11 ]
|
|
|
|