|
|
PROF. MWAKALILA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI - MNMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Sakai Mwakalila leo ameendesha Mkutano wa Tisa wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Kikao ambacho kimejadili na kupitia Maoteo ya bajeti ya Chuo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi kimefanyika katika Kampasi ya Kivukoni ambapo kimejadili Vipaumbele vya Chuo kwa mwaka 2024/25 ikiwa ni kuimarisha shughuli za Ufundishaji na ujifunzaji katika programu mbalimbali zitolewazo katika ngazi ya Cheti, diploma,Shahada na Shahada ya umahiri,
Kuendelea na utek ...
lezaji wa miradi ya Maendeleo iliyopitishwa katika bajeti ya mwaka 2023/2024.
Vingine vilivyojadiliwa ni ujenzi wa Madarasa 12 yenye uwezo wa kutumiwa na Jumla ya Wanafunzi 3600, kufanya ukarabati wa Miundombinu Chakavu ya Majitaka,Umeme,Barabara na Majengo, na kuimarisha Shughuli za Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Chuoni.
Kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi pia kimejadili Mpango wa Motisha kwa Wafanyakazi, ambao ukipitishwa na bodi utawasilishwa utumishi kwa hatua zaidi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
19.01.2024
Read more >
[ 2024-01-21 ]
|
|
|
|