RAIS MWINYI AKIPONGEZA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuendelea kuandaa Makongamano ya kuwaenzi waasisi wa Taifa na kuhakikisha historia ya nchi inatambulika kwa watu wa rika zote. Dkt.Mwinyi ameyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla katika kongamano la sita la kumuenzi Hayati Sheikh Abeid Karume lililoandaliwa na kufanyika katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Ka ... ume,Zanzibar. Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi amesema kuwa kuwepo kwa kongamano hilo kunatufanya turejee katika misingi iliyoanzishwa na Hayati sheikh Abeid Karume ya falsafa za Uwazi, Uadilifu,,Upendo, na ubunifu katika kulijenga Taifa. Dkt Mwinyi amesema Ni imani yake kuwa tutaziishi tunu hizi alizotuachia Hayati Mzee Abeid Karume ambazo zitabadilisha fikra zetu, Mienendo yetu na kuleta utendaji wenye kuboresha maisha ya Wananchi. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Mhe, Stephen Wasira amesema huwezi kuwa mzalendo bila kujua historia ya nchi yako na kuwa huwezi kuandika historia ya Zanzibar bila kumtajaMzee Karume. Awali akisoma taarifa ya Chuo, Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof.Shadrack Mwakalila amesema kuwa Chuo kinathamini na kutambua masuala ya Uzalendo, na Utaifa hivyo kimeweka kwenye mitaala yake masomo hayo ambayo kila mwanafunzi anayesoma Chuoni hapo hufundishwa pamoja na Taaluma nyingine. Profesa Mwakalila amesema kuwa Chuo kina utaratibu wa kuandaa makongamano kama haya ya kitaaluma kwa lengo la kujikumbusha misingi waliyoiweka ili kuhakikisha historia ya nchi inajulikana na kutambulika kwa watu wote. Pia Profesa Mwakalila amesema kwa sasa kampasi ya Karume ina jumla ya Wanafunzi 2400 kutoka wanafunzi 22 waliokuwapo wakati Kanpasi hiyo inaanzishwa jambo ambalo linaonesha wazi kwamba wazazi na Jamii wanatambua mchango na Elimu inayotolewa na chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Kongamano hilo limebeba dhamira kuu ambayo ni Falsafa za Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika kujenga Utaifa na Uzakendo kuelekea Uchumi wa Buluu Zanzibar. Kongamano hilo pia lilijadili Mada ndogo iliyosema; Amani na Unoja wa kitaifa katika utekelezaji wa Uchumi wa Buluu iliyowasilishwa na Waziri Kiongozi Mstaafu Mhe.Shamsi Vuai Nahodha na ya pili ni Mchango wa Wazalendo katika upatikanaji wa Maendeleo endelevu Zanzibar iliyowasilishwa na Profesa Palamagamba Kabudi. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 04.04.2024 Read more >
[ 2024-04-08 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam