|
|
DKT. SERERA AKIPONGEZA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWA KUENDELEA KUSIMAMIA MASUALA YA UONGOZI NA MAADILI.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Suleiman Serera amesema Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Kinamtafsiri kwa Vitendo Hayati baba wa Taifa Mwalimu JK, Nyerere maana tangu kuanzishwa kwa Chuo hiki bado kimeendelea kusimamia misingi ya utoaji wa Elimu inayozingatia masuala ya Uongozi na Maadili na ndiyo lilikuwa lengo la kuanzishwa kwake.
Dkt.Serera amesema hayo wakati ak?zungunza na Menejiment ya Chuo, pamoja na baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya kituo cha urithi wa Uko ...
bozi wa Afrika wakati wa kupitia rasimu ya hati ya Makubaliano ya Ushirikiano baina ya pande hizo mbili.
Dkt. Serera amebainisha baadhi ya maeneo ambayo yataingiwa katika ushirikiano huo ikiwemo kulinda na kuendeleza urithi wa ukombozi wa Afrika, kufanya tafiti, kutoa mafunzo na kuandaa machapisho kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu maadili na historia ya ukombozi wa taifa na Afrika kwa ujumla.
“Tukitumie zaidi Chuo hiki, maana ndiyo kimebeba jina la Muasisi wa Taifa letu, Hayari JK Nyerere, lakini pia Chuo hiki kinamtafsiri Mwalimu kwa Vitendo kwa kuwa Elimu inayotolewa hapa inamlazimu Mwanafunzi pamoja na kusoma kozi nyingine lakini kozi ya Uongozi na Maadili pia anaisoma,”alisisitiza Naibu Katibu Huyo Dkt Serera.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila ameahidi kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo kupitia kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, na kuhakikisha kuwa mashirikiano yanakuwepo kwa kuwa yaliainishwa katika hati ya makubaliano ya ushirikiano yanakigusa Chuo moja kwa moja na ni ya Muhimu.
Profesa Mwakalila amesisitiza kuwa masuala yote yaliyopo kwenye rasimu ya hati ya makubaliano ya Ushirikiano baina ya pande hizo mbili yana umuhimu na tija kwa Taifa.
Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
23.04.2024
Read more >
[ 2024-04-23 ]
|
|
|
|