MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATEMBELEA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERe
Mkuu wa wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ametembelea Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kukagua mradi wa Ujenzi wa Maktaba na Kumbi za mihadhara ambapo ameahidi kuzungumza na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ili mradi huo uweze kuendelea, kukamilika kwa wakati na kuleta tija kwa Taifa. Akizungumza na Wanafunzi, Wafanyakazi wa Chuo hicho mara baada ya kukagua mradi huo katika kampasi ya Kivukoni jijini Dar es Salaam Chalamila amesema mradi huo ni muhimu kwa historia ya Taifa kwani itapunguza changamoto ... ya msongamano inayowakabili wanafunzi kwa sasa kutokana na idadi ya Wanfunzi kuongezeka kila mwaka chuoni hapo. “Nimejionea Maendeleo ya Ujenzi wa mradi wa Maktaba na Kumbi za mihadhara jengo linaonekana ni imara japo kasi ya ujenzi ni ndogo nitafanya ushawishi kwa kukaa meza moja na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolph Mkenda ili fedha ya kuendelea na mradi ipatikane kwa haraka na kuepusha gharama mpya zinazoweza kujitokeza kwa ujenzi kutokamilika kwa wakati,”alisema Chalamila. Chalamila alisema, kama dira ya Chuo inavyosema kuwa ni kitovu cha utoaji wa Maarifa bora, Elimu na Mafunzo kuhusu ubunifu na uvumbuzi na kuendeleza Amani na Umoja wa Kitaifa ni kuwa ujenzi wa mradi huu utasaidia Wanafunzi kuweza kujisomea kwa nafasi na kumaliza changamoto ya msongamano . Aidha aliwataka wanafunzi wa chuo hicho kuendeleza Amani na umoja wa kitaifa ili wawe mfano kwa wengine Sambamba na kuwa na Maadili mema, kujiamini na kuwa wanawezakuwa mtu yeyote. Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof Shadrack Mwakalila amesema kukamilika kwa ujenzi huo wa Ukumbi wa Mihadhara utakuwa na uwezo wa uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 1000 pamoja na Maktaba itakayo kuwa na uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 2500 kwa wakati mmoja. Prof.Mwakalila amesema ni matamanio makubwa ujenzi wa Maktaba ukamilike kwa wakati maana udahili wa Wanafunzi unaongezeka kila mwaka hivyo kukamilika kwa Maktaba hiyo kutatoa fursa ya Wanafunzi kujifunza kwa nafasi. Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amewataka Wanafunzi wapambanie ndoto zao, na kuthamini Elimu wanayoipata Chuoni hapo kwani Taifa linawategemea. Hata hivyo Mhandisi Mjenzi wa Mardi huo Mwesigwa Ichwekeleza alisema kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 36 na kuwa changamoto ya fedha imekuwa ni kikwazo cha kushindwa kukamilisha kazi ya ujenzi huo kwa wakati, mpaka sasa fedha ambayo tayari imekwishalipwa ni Shilingi Bilioni 4 na kuwa ili mradi ukamilike unahitaji kiasi Zaidi ya Shilingi bilioni 14. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 04.06,2024 Read more >
[ 2024-06-07 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam