PROF. MWAKALILA AWATAKA WATUMISHI KUWAJIBIKA, NA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila Leo amezungunza na Watumishi wa Kampasi ya Kivukoni ya Chuo hicho ambapo amesema kuwa Katika mwaka wa fedha 2023-2024, chini ya miongozo ya Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chuo kimepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na Kutoa mafunzo katika fani mbalimbali za kitaaluma kwa kiwango cha Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili, Kutoa mafunzo ya uongozi, maadili na uzalendo, Kufa ... ya utafiti zenye kutatua changamoto mbalimbali katika kijamii, Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa sekta ya umma na sekta binafsi; na Kuendesha mafunzo ya elimu ya kujiendeleza. Amesema Katika Kampasi ya Kivukoni, Chuo kimeboresha miundombinu katika mabweni ya Wanafunzi, madarasa pamoja na ofisi za Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kukarabati nyumba za Wafanyakazi, kanteeni. Ujenzi wa maktaba kubwa yenye uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 2,500 pamoja na ukumbi wa midahalo wenye uwezo wa kuchukua watu 1000. Ujenzi wa mabweni yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1,536 katika Kampasi ya Karume na kuwa ujenzi huo upo 80%. Ujenzi wa madarasa na jengo la Utawala katika Kampasi ya Pemba na kuwa madarasa yamekamilika na yameanza kutumika. Profesa mwakalila amesema Udahili umeogezeka na kufikia wanafunzi 14,134 kwa mwaka huu wa masomo 2023/2024, Chuo kimewezesha kuwalipia ada za mafunzo watumishi zaidi ya 50 katika ngazi mbalimbali za masomo ikiwemo Shahada ya Uzamivu, Shahada ya Umahiri, Shahada ya Awali. Chuo kimetoa semina ya mbinu za ufundishaji kwa wahadhiri wote kwa Kampasi zote tatu na pia Chuo kimeongeza idadi ya wahadhiri wenye shahada ya uzamivu (PhD) na kufikia wahadhiri wenye PhD zaidi ya 50 mwaka 2024. Mkuu huyo wa Chuo amesema Mkutano huo ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika tarehe16-23 Juni kila mwaka, ambapo pia amewataka Wakurugenzi, Wativa, Wakuu wa Idara na Vitengo kufanya vikao na watumishi walio chini yao kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua changamoto walizonazo kazini. Prof. Mwakalila amesema idadi ya watumishi imeongezeka baada ya kupata kibali cha ajira za watumishi zaidi ya 90 na kufanya jumla ya watumishi wa kudumu kuwa 350. Pia Chuo kimekuwa kikishiriki katika mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Tekinolojia na Ubunifu chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Pia Chuo kimeshiriki kwenye mashindano mbalimbali ya michezo katika ngazi ya kitaifa (SHIMIVUTA na SHIMMUTA) kwa mafanikio makubwa. Pia amewasisitiza watumishi kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wadau, wakiwemo Wanafunzi, kufanya kazi kwa juhudi na Maarifa, kuwa wabunifu na kuwajibika kwa kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma. Pia amewataka Watumishi kutambua Dira ya Chuo ni kuwa kitovu cha utoaji wa Maarifa bora kwa kutoa Elimu na Mafubzo kuhusu ubunifu na Uvumbuzi na Kuendeleza Amani na Umoja wa Kitaifa. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Masoko CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NY Read more >
[ 2024-06-20 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam