|
|
PROF. MWAKALILA AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI KUONGOZA KWA NIDHAMU NA KUSOMA KWA BIDII
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amewapongeza Viongozi wapya wa Serikali ya Wanafunzi kwa kuchaguliwa na kuaminiwa hivyo amewataka wahakikishe wanatimiza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu , miongozo, na sheria zilizopo.
Prof. Mwakalila amesema hayo leo wakati wa Semina Elekezi ya kuwajengea uwezo Viongozi Wapya wa Serikali ya Wanafunzi kwa Mwaka 2024/2025 kupitia kurugenzi ya huduma za Wanafunzi ya Chuoni hapo.
Mkuu huyo wa Chuo amewasisitiza Viongozi hao kushirikisha viongozi mbalimbali katika kuf ...
nya maamuzi katika mambo mbalimbali na siyo kujiamulia au kufanya maamuzi wao wenyewe.
" Msijiamulie mambo wenyewe wenyewe jitahidini kushirikisha Viongozi wengine ili maamuzi yatakayofanyika yawe na tija kwa Chuo na Taifa kwa ujumla.” Alisisitiza Prof. Mwakalila
Prof. Mwakalila amewataka pia Viongozi hao wa Wanafunzi kudumisha Amani, Umoja, Upendo na mshikamano katika maisha yao ya kila siku.
Amewakumbusha kuwa pamoja na kwamba wao ni viongozi wa Wanafunzi,lakini jukumu lao la msingi ni kusoma na kufanya vizuri katika masomo yao.
Kupitia semina hiyo Viongozi hao wa Serikali ya Wanafunzi watajifunza kuhusu dhana ya Uongozi na Utawala bora,kanuni, taratibu na Matumizi ya fedha za Umma, Migogoro, utatuzi na wajibu wa Serikali ya Wanafunzi, Uongozi bora, Maadili na Wajibu wa Kiongozi bora, Mawasiliano na Matumizi ya Muda na kazi za dawati la Jinsia.
Katika tukio lingine, Prof. Mwakalila pia amewapongeza Vijana wa Skauti kwa kuwa mstari wa mbele katika kujitolea zaidi katika shughuli mbalimbali za kitaifa, ambapo tangu kuanzishwa kwa Skauti mwaka 2019 hadi 2024 zaidi ya mafanikio 26 yameweza kupatikana.
Mkuu wa Chuo pia ameridhia ombi la kuwepo kwa bodi ya Skauti kwa lengo la kuongeza tija na kuleta msukumo wa skauti katika kufikia malengo na mipango ambayo Chama hicho cha Skauti imejiwekea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
19.06.2024
Read more >
[ 2024-06-20 ]
|
|
|
|