|
|
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHAPOKEA MSAADA WA JEZI ZA MICHEZO KUTOKA HALOTEL
Naibu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anaesimamia Utawala, Fedha na Mipango Dkt Evaristo Haule Leo amepokea msada wa vifaa vya michezo mbalimbali zikiwemo jezi na Mipira vyenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili, kutoka kampuni ya simu ya Halotel ambapo ameshukuru msaada huo na kusema kuwa msada ulitolewa utatumika kama ilivyokusudiwa.
Ak?zungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, Dkt Haule amesema, Chuo kinaamini kuwa pamoja na kupokea msaada huo lakini hiyo ni ishara tosha ya kuwepo kwa ushirikiano mzuri, umoja, mshikamano ...
a undugu kati ya MNMA na Kampuni hiyo ya simu ya Halotel na kusisitiza kuwa ushirikiano huo uendelee.
“Michezo inawaleta watu pamoja, michezo ni afya, michezo ni Upendo kwa hiyo hiki mlichokifanya halotel cha kukabidhi jezi na mipira kwa Taasisi yetu kinaendeela kutuweka pamoja.”alisisitiza Dkt. Haule.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kibiashara wa Kampuni ya Simu ya hallotel Wilaya ya Temeke na kinondoni Jerome Shayo amesema Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni Wadau wao wakubwa kupitia Wanafunzi ambao wanatumia mtandao huo wa simu wa Hallotel, ambapo gharama zake ni nafuu na wanafunzi wamekuwa wakimudu gharama hizo.
Shayo amesema Jezi zilizokabidhiwa leo ni zile zitakazotumika kwenye Mchezo wa jezi Mpira wa Nyavu (Voleyball), jezi Mpira wa Miguu wa Wanaume (Football) na jezi za Mpira wa Pete (Netball), pamoja na Mipira Mitatu ya michezo husika.
Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
23.08.2024
Read more >
[ 2024-08-26 ]
|
|
|
|