PROF. HARUNI JEREMIA MAPESA APOKELEWA RASMI CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Mkuu mpya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Jeremia Mapesa leo amepokelewa na Menejimenti ya Chuo baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya Kuiongoza Taasisi hiyo ambapo ameahidi kushirikiana na Bodi ya Chuo chini ya Mwenyekiti wake Mhe.Stephen Wasira, Menejimenti na Wafanyakazi wote kwa lengo la kuhakikisha Taasisi inakidhi matarajio ya Taifa. Akizungumza na Menejimenti ya Chuo hicho Baada ya kupokelewa Prof. Mapesa amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kumteua huku akiahid ... kufanya kazi kwa Weledi. Prof Mapema amesisitiza kuwa ili kufikia malengo lazima sheria, kanuni, tarataibu na miongozo ya utumishi wa Umma ifuatwe wakati wote wa kutekeleza majukumu ya kila siku. “ Uongozi ni kufanya kazi kwa pamoja yaani ( team work), hivyo ninawaahidi kuwa niko hapa kuhakikisha tunashirikiana kwa weledi katika kufanya kazi na kutoa maamuzi kwa pamoja na kwa karibu ili kutimiza malengo ya Taasisi pamoja na kutekeleza na kukidhi matatajio ya Wadau wetu na Taifa kwa ujumla,” alisisitiza Prof. Mapesa. Katika hatua nyingine Prof. Mapesa amefanya ziara ya kutembelea baadhi ya ofisi na mazingira ya chuo kujionea utendaji kazi Chuoni hapo. Aidha, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Chuo ambaye ni Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe, akikabidhi ofisi kwa Mkuu wa Chuo mpya, amefafanua kuhusu muundo na majukumu ya Chuo na kuahidi ushirikiano katika utekelezaji wa kazi za kwa ustawi wa Chuo na taifa kwa ujumla. Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Menejimenti , Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Evaristo Haulle amemuahidi Mkuu huyo mpya wa Taasisi ushirikiano wa dhati kutoka kwa Watumishi wakati wote atakapokuwa anatimiza majukumu yake Imetolewa na: KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE 14.11.2024 Read more >
[ 2024-11-20 ]
Visitors Counter
Flag Counter
Collaboration

TCU Link

NACTE Link
NECTA Link
ZHELB Link
HELSB Link
MoEST Link
MoEZ Link
Social Networks
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter
Contact us
Hotline : +255 (22) 2820041/47
P.O.BOX : 9193 Dar es Salaam,TANZANIA
Email : rector@mnma.ac.tz
Location : Kivukoni Dar-es-salaam