|
|
PROF. HARUNI MAPESA AFANYA ZIARA KATIKA KAMPASI YA KARUME ZANZIBAR.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Haruni Jeremia Mapesa amefanya ziara ya kwanza katika kampasi Karume ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo visiwani Zanzibar kwa lengo la kukutana na kuzungumza na Watumishi huku akiendelea kuahidi kushirikiana na watumishi katika kuhakikisha chuo kinafikia malengo yake ya msingi ya kufundisha, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa Kitaalamu.
Akizungumza jana wakati wa kikao cha pamoja na Wafanyakazi na viongozi waliopo katika Kampasi hiyo ya Karume, Prof. Mapesa amebinisha kuwa ...
atahakikisha Fikra, Maono na Falsafa za baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere zinaendelea kuzingatiwa.
huku akiwasisitiza Viongozi na Watumishi wote kufanya kazi kwa pamoja na kwa mshikamano.
Swali akimkaribisha Mkuu huyo wa Chuo, Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amesema Prof.Mapesa ni kiongozi bora kwani anawasifu uliojitosheleza kuongoza Taasis hiyo.
Akitoa neno la shukrani Naibu Mkuu wa Chuo upande wa Utawala Dkt.Evaristo Haule amemuahidi Mkuu wa Chuo kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha utendaji kazi mzuri wenye kuzingatia Kanuni,Sheria ,Taratibu na Miongozo ya Serikali.
Katika ziara hiyo Mkuu wa chuo ameambatana na Wasaidizi wake ambao kwa pamoja walitembelea eneo la Mradi wa Mabweni ya Wanafunzi na maeneo mengine ya chuo ili kuweza kuyafahamu vizuri mazingira ya Kampasi hiyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
20.11.2024
Read more >
[ 2024-11-22 ]
|
|
|
|