|
|
PROF MAPESA AAHIDI KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA KWA KUZINGATIA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Jeremia Mapesa leo amekutana na kuzungumza na Wafanyakazi wa kampasi ya Kivukoni jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujitambulisha ambapo amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa Kumteua huku akiahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi
Akizungumza na Wafanyakazi hao Prof Mapesa amesisitiza suala la Viongozi na Wafanyakazi kufanya kazi kushirikiana,kwa haki, Weledi, na kuzingatia Maslahi ya Wafanyakazi ili kuyafanya maisha mahala Pa kazi yawe na fu ...
aha.
Prof. Mapesa amewapongeza Wafanyakazi kwa kuchapa kazi kwa bidii na hivyo kimesaidia Chuo kujulikana, Kuvutia Wadau wa Maendeleo huku akisema kuwa kauli Mbiu yetu ni ,” Umoja ni Ushindi”.
“Nimekuja kufanya kazi ya Mkuu wa Chuo, nitajitahidi kufuata kanuni, taratibu, sheria na Miongozo ya Utumishi wa Umma ili kufikia matarajio ya Wadau,”Alisitiza Mkuu wa Chuo.
Prof. Mapesa pia ametumia fursa hiyo kumpongeza mtangulizi wake ambaye ni Prof Shadrack Mwakalila kwa uongozi wake wa miaka 10 (kuanzia 2014- 2024) ambaye kwa sasa amemaliza muda wake.
Amewataka Watumishi kujitokeza kwenye sherehe za Mahafali ambazo zitafanyika katika Kampasi za Chuo hicho kati ya tarehe 29 Kivukoni, 02 Karume na tarehe 04 Kampasi ya Pemba mwaka huu maana huo Ndiyo muda sahihi wa kujipongeza na kujitafakari pamoja.
Akizungumza awali kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Chuo,Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof Richard Kangalawe alisoma wasifu wa Mkuu huyo mpya na kueleza kuwa ni Wasifu unaojitosheleza.
Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
26.11.2025
Read more >
[ 2024-11-27 ]
|
|
|
|