|
|
KUSANYIKO LA WAHITIMU - MNMA - LAFANYIKA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa leo amepokea na ameahidi kushughulikia Changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na kusanyiko la baraza la Wahitimu(Alumni), kupitia taarifa waliyoisoma wakati wa kusanyiko hilo hii leo.
Akizungumza wakati wa kusanyiko hilo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amewaeleza Wahitimu kuwa ili kufanikisha majukumu ya baraza hilo Chuo kimeahidi kuwepo na mkakati Maalumu wa Kushughulikia a Changamoto za ...
baraza la Wahitimu ikiwa ni pamoja na kuwa na
Liaison Officer) ili aweze kusajili na kutunza taarifa za wahitimu. Pia Chuo Kimeahidi kuanzisha ofisi maalumu kwa ajiliya kushughulika na masuala ya kusanyiko la wahitimu ili kuboresha zaidi ufanyikaji wa Kusanyiko hiko.
Amesema Ofisi hiyo itakuwa ni kiungo muhimu kati ya Kamati Tendaji ya Kusanyiko na Menejimenti ya Chuo.
Awali akisoma hotuba ya Kusanyiko la baraza la wahitimu, katibu Mtendaji wa baraza hilo Jumanne Muruga ameahidi kuwa Viongozi wa kusanyiko hilo wataendelea kushirikiana na Menejimenti katika kuhakikisha Mafanikio ya Chuo yanafikiwa kwa kuwa Wahitimu Ndiyo Mabalozi wazuri wa kukisemea Chuo katika Jamii.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
28.11,2024
Read more >
[ 2024-11-30 ]
|
|
|
|