|
|
MZEE WASIRA AWATAKA WAHITIMU KAMPASI YA KARUME KUJIENDELEZA
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mhe. Stephen Wasira amewaasa wahitimu wa chuo hicho kupenda kujiendeleza kwa Maslahi mapana ya Taifa na jamii kwa ujumla .
Mzee Wasira ameyasema hayo leo wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Karume Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Kampasi hiyo eneo la Bububu visiwani Zanzibar.
Mwanasiasa huyo Mkongwe amewataka Wahitimu kuhakikisha
wanakuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza chuo huko wanakokwenda,Pia wajitahidi kujiendeleza kielim ...
na wasiridhike tu na Elimu waliyoipata Chuoni hapo.
Aidha,Mzee Wasira ameongeza kuwa wahitimu hao wamepikwa vizuri katika fani mbalimbali na kuongezewa mafunzo ya Uongozi, Maadili na Utawala bora ili waweze kuleta tija katika utendaji wao kwenye sekta mbalimbali za umma na binafsi ambazo watabahatika kupangiwa.
Awali akisoma hotuba ya kuelezea Mafanikio ya Chuo ,Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Harun Mapesa amesema kuwa idadi ya wanafunzi wanaohitimu katika Chuo hicho imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka jambo ambalo linaonyesha kuwa chuo kinaaminika na jamii kwa kutoa Elimu iliyo bora na yenye viwango vinavyokubalika.
“Nawashukuru Wazazi kwa kuendelea kukiamini chuo hiki na ninawaomba waendelee kufanya hivyo kwani chuo kina ubora unaotambulika kitaifa na kimataifa,”Alisisitiza Prof. Mapesa.
Prof. Mapesa amewataka Wahitimu hao kutumia ujuzi na Maarifa waliyoyapata katika kuhakikisha wanatatua changamoto mbalimbali zilizopo katika Jamii.
Jumla ya wahitimu 1268 kati ya hao, 791 sawa na asilimia 62 ni wasichana na wavula 477 sawa na asilimia 38 wamehitimu kozi mbalimbali katika Chuo hicho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
2.12.2024
Read more >
[ 2024-12-03 ]
|
|
|
|