|
|
WASIRA AWATAKA WAHITIMU KAMPASI YA PEMBA KUENDELEZA MAADILI
Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mzee Stephen Wasira amewataka Wahitimu wa Chuo hicho Kampasi ya Pemba kuendeleza Maadili mema waliyojifunza wakati wa wakiwa Chuoni hapo.
Mzee Wasira amesema hayo leo Pujin- Pemba wakati wa Mahafali ya 2 ya Kampasi hiyo ambapo Wahitimu 230 wametunukiwa vyeti katika Kozi mbalimbali.
Aidha, Mzee Wasira amewataka Wahitimu kuwa mfano bora katika eneo la Maadili kwa kuwa Chuo walichohitimu kimebeba jina la Baba wa Taifa ambaye ndiye Mwanzilishi na malengo ya Chuo tangu kuanzoshwa kwa ...
e ni kutoa Elimu ya Maadili hivyo ni vyema wakaendeleze Maadili mema kwa Maslahi mapana ya Taifa..
Mzee Wasira pia amempongeza Prof. Haruni Mapesa kwa kuaminiwa na kiteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kukiongoza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Awali akisoma hotuba ya kuelezea Mafanikio ya Chuo ,Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Harun Mapesa amesema kuwa idadi ya wanafunzi wanaohitimu katika Kampasi ya Pemba inaongezeka mwaka hadi mwaka, na hii inaonesha kuwa Wazazi na Walezi wameendelea kukiamini chuo kwa kutoa Elimu iliyo bora na yenye viwango vinavyokubalika.
“Nawashukuru Wazazi kwa kuendelea kukiamini chuo hiki na ninawaomba waendelee kufanya hivyo kwani chuo kina ubora unaotambulika kitaifa na kimataifa,”Alisisitiza Prof. Mapesa.
Prof. Mapesa amewataka Wahitimu hao kutumia ujuzi na Maarifa waliyoyapata katika kuhakikisha wanatatua changamoto mbalimbali zilizopo katika Jamii.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
4.12.2024
Read more >
[ 2024-12-05 ]
|
|
|
|