|
|
MNMA YASHIRIKI MAZIKO YA DKT. GODWIN KAGANDA
Naibu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anaesimamia Mipango, Fedha na Utawala, Dkt Evaristo Haule ameshiriki maziko ya Dkt Godwin Kaganda ambayo yameanyika leo tarehe 24.12.2024 katika kijiji cha Kanyigo- Kigarama , Wilayani Bukoka mkoani Kagera.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Dkt Haule amemuelezea Dkt Godwin Emmanuel kaganda kuwa alikuwa ni mchapakazi, Mnyenyekevu na aliyesimamia miongozo, taratibu na Sheria za Utumishi wa Umma wakati wote alipokuwa akitumiza majukumu yake.
Wakati w ...
uhai wake Dkt. Godwin Kaganda amewahi kufanya kazi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu akiwa na Cheo cha Naibu Mkuu wa Chuo anaeshughulikia Mipango, Utawala na Fedha kwa mwaka 2019 hadi mwaka 2022.
Bodi ya Chuo, Menejimenti, Wafanyakazi na Wanafunzi wote wanatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na Marafiki kwa msiba huo.
Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.Aaamina.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
24.12.2024
Read more >
[ 2024-12-27 ]
|
|
|
|