|
|
PROF. MAPESA AKUTANA NA KANSELA WA UBALOZI CHINA WAAHIDI KUSHIRIKIANA KATIKA TAALUMA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Mapesa leo amekutana na kufanya mazungumzo na Kansela wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Xu Sujiang kutoka idara ya kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomonisti cha China(IDCPC) ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuendeleza ushirikiano katika masuala ya Kitaaluma na Kimaendeleo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Chuo kampasi ya Kivukoni jijini Dar es Salaam ambapo Kansela Sujiang alitumia fursa hiyo Kumpongeza Mkuu huyo wa Chuo mpya kwa kuaminiwa na ...
uteuliwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Chuo na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali.
Prof Mapesa amesema Chuo kipo tayari kushirikiana na nchi ya China katika masuala mbalimbali ikiwemo ya kitaaluma,huku akieleza kuwa Chuo kina
kampasi tatu ambazo ni Kampasi ya Kivukoni, Kampasi ya Karume - Zanzibar na Kampasi ya Pemba ambapo alieleza kuwa zipo baadhi ya Changamoto ikiwemo upungufu wa Madarasa,hosteli za Wanafunzi na ofisi za Walimu kwa Kampasi ya Karume na Pemba hivyo Chuo kinahitaji ushirikiano kwenye maeneo hayo.
Profesa ameshukuru kuteuliwa na kuongoza Chuo hiki Chenye historia kubwa na iliyotukuka siyo tu ndani ya nchi Bali hata kimataifa.
Aidha aliongeza kuwa Falsafa, Itikadi na dhamira ya Baba wa Taifa Julius Nyerere katika kuliendeleza Taifa lake inashabihiana sana na Falsafa na Maono ya baba wa Taifa la China Mao Tse Tung.
Prof Mapesa amesema lengo la kuanzishwa kwa Chuo ilikuwa ni kufundisha viongozi ambao wanashika Madaraka katika nafasi mbalimbali katika nchi kazi ambayo bado Chuo Kinaendelea kuifanya kwa kutoa Mafunzo ya Uongozi na Maadili kwa Viongozi mbalimbali.
“mwakani nchi yetu itajngia kwenye uchaguzi, kwa hiyo sisi tutatakiwa kuwafundisha Wadau watakaoshiriki Mchakato wa Uchaguzi, na viongozi wapya watakaochaguliwa kuongoza kwa kuwa sisi ni Chuo cha Uongozi na Maadili,”alisisitiza Prof. Haruni Mapesa.
Profesa Mapesa alimueleza kansela Sujiang kuwa Chuo kinahitaji kusaidia katika kupata wataalamu ambao watawashauri vijana mbalimbali wanahitumu katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika masuala ya kiteknolojia, jinsi ya kujiajiri na kujipatia kipato.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe na Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Mipango, Utawala na Fedha Dkt. Evaristo Haulle.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
30.12.2024
Read more >
[ 2024-12-30 ]
|
|
|
|