|
|
BENKI YA NMB YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Jeremia Mapesa ameikaribisha benki ya NMB kuja kuwekeza Chuoni hapo kwa kutumia rasilimali ya Ardhi iliyopo Chuoni hapo.
Prof Mapesa ameyasema leo baada ya kukutana na Meneja Mwandamizi wa Mahusiano wa NMB Rachel Kissui ambapo pamoja na mambo mengine Prof Mapesa amesema kwa sasa Chuo kinahitaji kuongeza mkakati wa ndani wa kuongeza mapato hivyo uwekezaji wowote utakaofanywa na NMB utakuwa na tija kwa Chuo.
Mkuu huyo wa Chuo pia ameiomba benki kushirikiana na Chuo katika maeneo mb ...
limbali ikiwemo eneo la kozi fupi, ushauri wa kitaalamu, Utafiti, Uongozi na Maadili katika maeneo ya ubobezi ya Chuo na kuwa NMB imeahidi kushirikisha katika maeneo hayo kwa kadri ya mahitaji
Mkuu huyo wa Chuo ameieleza NMB kuwa idadi ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hivyo benki ione namna bora ya kukisaidia Chuo katika eneo hilo.
Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Mahusiano Rachel Kissui amekishukuru Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa Ushirikiano ambao Chuo imekuwa ikionesha kwa benki hiyo ya NMB.
Kissui amesema benki hiyo pia imempongeza Prof. Haruni Mapesa kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo hicho hivyo amemhakikishia ushirikiano.
Kissui amesema benki pia inautaratibu wa kurudisha kwenye jamii kiwango cha asilimia moja ya faida ambayo benki inaipata ambapo benki huwa inajikita zaidi katika kusaidia eneo la Afya na Elimu.
Kissui amemhakikishia Mkuu huyo wa Chuo kuwa benki ya NMB iko tayari kushirikiana na Chuo katika masuala mbalimbali ikiwemo ya kifedha na kitaaluma.
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
10.01.2025
Read more >
[ 2025-01-13 ]
|
|
|
|