|
|
PROFESA MAPESA APONGEZA WANAFUNZI MNMA KWA USHINDI SHIMIVUTA
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa. Haruni Mapesa jana ijumaa tarehe 7.02.2025 amewapongeza Wanafunzi na Makocha walioshiriki Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Kati Tanzania -Shimivuta – ambayo ilifanyika mwaka jana katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Profesa Mapesa amesema Chuo kitaendelea kuongeza bajeti sambamba na kuboresha miundombinu ya Michezo mbalimbali ambayo Chuo imekuwa ikishiriki, huku akisisitiza kuwa Wanafunzi wanaposhiriki Michezo vizuri inaimarisha akili, inaimarisha ustahmilivu na kuongeza ...
haiba ya mtu.
Mkuu huyo wa Chuo amesema pamoja na Wanafunzi kurudi na ushindi wa kombe la mchezo wa Mpira wa wavu (Volleyball), sasa amewataka Wanafunzi kuhakikisha wanajipanga na kuongeza vikombe vingi, na kuwa ili kufikia azma hiyo lazima mazoezi yaanze sasa ili mwakani tupate ushindi kwani ushindi ni heshima na Chuo kitaheshimika.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Utawala, Fedha na Mipango Dkt Evaristo Haulle ameeleza kuwa ajenda ya msingi ya Chuo ni Taaluma lakini Michezo inafanyika ili kuwa imara ki afya na pia kusaidia mambo mengine kwenda sawa.
Naye Prof. Richard Kangalawe Naibu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu amesema michezo husaidia Wanafunzi kufanya vizuri katika masomo, lakini pia Chuo kitazingatia kuwa hakutakuwa na mwingiliano wa ratiba za masomo na mazoezi ili kutoa fursa kwa Wanafunzi Wanamichezo kupata nafasi ya kufanya mazoezi vyema.
Akitoa neno la Shukrani kwa Uongozi wa Chuo Mkurugenzi wa huduma za Wanafunzi Ukende Mkumbo amesema idara imepokea Maelekezo ya kuhakikisha Mashindano yajayo watafaya vizuri huku wakiipongeza Menejimenti kwa ushirikiano kuanzia mwanzo wa mashindano hadi mwisho.
Mkumbo alibainisha kuwa Wanafunzi 53 walishiriki Michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Wavu, Mpira wa Miguu, Kuvuta Kamba, Puli la Mezani (Pool Table), Netiboli na Mpira wa Kikapu.
Wanafunzi waliofanya vizuri katika Michezo hiyo wamepata motisha na vyeti vya kuwatambua ushiriki wao.
Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU
08.02.2025
Read more >
[ 2025-02-16 ]
|
|
|
|